Jinsi ya Kufanya Smartphone Yako Idumu Kwa Muda Mrefu

Kama unataka simu janja yako idumu kwa muda mrefu soma hapa
Jinsi ya kufanya simu idumu Jinsi ya kufanya simu idumu

Binafsi nimeshatumia simu nyingi sana na ukweli kwenye simu zote ambazo nimewahi kutumia kwa kipindi chote cha utu uzima wangu ni simu moja tu ambayo sina kwa sasa hivi.. Simu zote nilizo nazo ziko kwenye hali nzuri sana na naweza kuuza na kupata pesa nzuri sana kutokana na hali ya simu hizo.

Najua kuna watu wengi sana wanapambana na hali ya kutoweza kudumu na simu kwa muda mrefu na hii sio mara zote inasababishwa na bahati mbaya. Ndio maana leo nimeamua kukuletea makala yenye hatua ambazo zimenisaidia sana mimi kuweza kudumu na simu zangu zote zikiwa kwenye hali nzuri. Natumaini mpaka mwisho wa makala hii utaweza kujifunza njia za kufuata ili kuweza kudumu na simu yako kwa muda mrefu.

1. Nunua Simu Kulingana na Aina Yako ya Kazi

Najua kichwa cha habari kimekushangaza kidogo lakini wala usishtuke kwani hiyo ni pointi ya msingi sana ambayo nitaifafanua kama ifuatavyo. Kama umefikiria kwenda kununua simu ni vyema kwanza ujijue wewe mwenyewe ni mtu wa aina gani, hii ni muhimu kwani zipo simu za aina nyingi sana sokoni simu zilizotengenezwa kwa Plastiki, zilizotengenezwa kwa Glass na zilizotengenezwa kwa chuma chepesi. Sasa wakati unataka kununua simu usiangalie tu sifa, bali angalia na material ya simu kwani kama wewe unafanya kazi ngumu na ukaenda kununua simu yenye Material ya Glass basi ni wazi simu hiyo haitoweza kudumu kwa muda mrefu.

Advertisement

Vilevile ni muhimu kukumbuka, Wengi wetu tunatumia muda mwingi sana kazi kuliko sehemu nyingine yoyote hivyo sidhani kama utakuwa na raha ya kuwa na simu ambayo huwezi kuitumia mahali unapo hitaji, Hivyo basi ni muhimu kuzingatia hili wakati unafikiria kununua simu kwani litakusaidia sana.

2. Tumia Simu Mahali Husika

Pointi hii inaendana na Point hapo juu, kama umesha nunua simu ambayo kwa namna moja ama nyingine haiendani na aina ya shughuli unayofanya basi hatua hii inaweza kukusaidia. Hakikisha simu yako unaitumia kwenye maeneo husika tu, Jiepushe kutumia simu maeneo ya hatari kama barabarani, Chooni, wakati unafanya kazi au wakati wa Michezo au Mazoezi. Najua kuwa simu za mikononi ni sehemu ya maisha yetu lakini ni vyema kuwa makini usije kupata hasara na kupoteza sehemu ya maisha yako.

Kwa wale ambao tayari wanasimu zenye ubora pia ni muhimu kufuata hatua hizi kwani zitakusaidia kudumu na simu yako kwa muda mrefu sana niamini kwa hilo.

3. Usinunue Simu Kubwa Kama Una Mikono Midogo

Mara nyingi watu wengi wanao angusha au kuibiwa simu kizembe ni wale wenye mikono midogo hii inasababishwa na kutoweza kuishikilia vizuri simu yako hivyo huwa ni rahisi sana kutoka mkononi. Kwangu binafsi mimi ninayo kanuni ambayo inafanya nione simu ni kubwa sana kwangu au inanifaa, unachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yako kisha shikilia huku umekunja vidole vyako vyote, sasa kikawaida inatakiwa atlist vidole viwe vimekaribiana angalau viache nusu inch au nchi moja. Angalia picha hapo chini.

Sasa kama unayo simu ambayo imekuwa ngumu sana hata vidole kukaribiana basi inawezekana kabisa simu hiyo ni kubwa sana ulinganisha na mkono wako. Kama tayari unayo simu ambayo ni kubwa sana kwenye mkono wako basi unachoweza kufanya ni kununua kava la mpira ambalo itakuwa na uwezo wa kung’ang’ania kwenye mkono wako pale unapokuwa umeshika simu yako, hiyo itakusaidia pia hata pale mtu anapo taka kunyakuwa simu yako.

4. Badilisha Screen Protector Kila Baada ya Muda

Screen protector zimetengenezwa maalum kwaajili ya kulinda vioo vya simu, lakini wakati mwingine usipokuwa makini screen protector inaweza kusababisha kioo cha simu yako kupasuka kwa urahisi zaidi. Mara nyingi screen protector inapo shikana sana na kioo cha simu yako kwa muda mrefu sana huwa kama sehemu ya kioo hicho, hivyo basi mara nyingi pale simu inapo anguka na endapo screen protector hiyo imekuwa kwenye simu yako kwa muda mrefu, kioo cha simu yako hupasuka sambamba na screen protector na hiyo ni kutokana na mshikamano wa muda mrefu wa screen protector na kioo cha simu yako.

Ni muhimu kubadilisha screen protector mara kwa mara inapobidi, pia hakikisha unanunua screen proctector ambayo inaweza kulinda vizuri simu yako.

5. Usitumie Kava la Plastiki Ngumu

Kila mtu anapenda simu yake ionekane vizuri, lakini kuna wakati urembo wa kupindukia ndio chanzo cha maradhi mengi ya kujitakia.. Vilevile kwenye upande wa simu ni hivyo hivyo. Hakikisha simu yako inakuwa simu smart na sio yenye urembo wa kupitiliza, pia hakikisha hutumii kabisa kava la plastiki ngumu kwani makava haya huwa na mtindo wa kuchubua simu na ni rahisi sana kufanya simu ivunjike pale inapo anguka.

Badala yake tumia kava lenye mpira kwani litakusaidia sana hasa pale simu yako inapo anguka itaweza kudunda kama itaanguka kwa muelekeo fulani. Pia kama nilivyosema kwenye pointi hapo juu kava la mpira litasaidia kuzuia simu yako isiteleza na kuzuia simu yako kuanguka kwa urahisi, vilevile kuwa makini na hakikisha unachagua kava la mpira lenye material mazuri.

6. Pendelea Kufanyia Usafi Simu Yako

Hivi mara yako ya mwisho kusafisha simu yako ni lini..? Ni kweli kuwa tunapenda simu zetu lakini tunasahau pia simu zinabeba uchafu sana na pengine ni moja kati ya sababu za simu hizo kuharibika kwa haraka. Mara nyingi utakuta mtu anafuta TV, Kompyuta na vitu vingine vya kieletroniki lakini mara chache sana utakuta mtu anafuta simu yake bila kutumia kitambi au tumbo…

Kufuta simu yako na uikagua ni moja kati ya vitu muhimu sana, hii itakusaidia kujua baadhi ya matatizo ya simu yako na pia itasaidia kufanya simu yako ifanye kazi vizuri. Mara nyingi unaweza kukuta kila siku mtu anakwambia hakusikii vizuri lakini kumbe tatizo ni simu yako inakuwa na uchafu mwingi kwenye kitundu cha kinasa sauti au mic. Ni muhimu kuhakikisha unakagua simu yako angalau mara mbili kwa mwezi hiyo itakusaidia sana kuweza kudumu na simu yako kwa muda mrefu.

Na hizo ndio njia ambazo zinaweza kukusaidia kudumu na simu yako kwa muda mrefu, Kama una swali au maoni unaweza kutuandikia kupitia maoni hapo chini, pia soma hapa kama unataka kujua hatua za kufuata kama unataka kwenda kununua simu kariakoo au sehemu nyingine na kuhakikishia utanishukuru baada ya kusoma makala hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use