Jinsi ya Kujua Mtu Anayeshika Simu Yako Bila Wewe Kujua

Jifunze hapa hataua za kujua mtu anayeshika simu yako bile wewe kujua
Jinsi ya kujua mtu anayeshika simu yako bila wewe kujua Jinsi ya kujua mtu anayeshika simu yako bila wewe kujua

Kati hali ya usalama ni wazi kuwa watu wengi sana wanatabia za kushika simu za watu bila kupewa ruhusu. Tabia hii ni kubwa sana miongoni mwetu kiasi kwamba leo imebidi kuja na makala hii ya jinsi ya kujua mtu anaeshika simu yako bila wewe kujua. Mbali na hayo njia hii pia inaweza kuwa msaada mkubwa pale unapopoteza simu yako kwani itakusaidia utaweza kujua aliyechukua simu yako moja kwa moja.

Njia hii ni rahisi sana na sidhani kama nitakuboa kwa maelezo marefu kwani ni hatua chache sana unazotakiwa kufuata ili kuweka ulinzi huu muhimu na rahisi kwenye simu yako. Kwa kuanza leo nitakuleta njia hii kupitia simu ya android alafu baadae nitakufahamisha njia hii kwenye simu za mfumo wa iOS, Basi bila kupoteza muda twende tukajifunze njia hii.

Kwa kuanza unacho kihitaji ni pamoja na simu yenye mfumo wa Android, pia unahitajika kuwa na internet angalau MB 100 kwani tunenda kuzitumia kupakua app kupitia soko la Play Store, kama tayari unavyo vitu vyote hivyo basi unaweza kuendelea kwenye hatua inayofuata.

Advertisement

Hatua ya kwanza, ingia kwenye soko la Play Store kisha download App inayoitwa Intruder Selfie, unaweza kupata app hiyo kwa kutumia link hapo chini na utapelekwa kwenye soko la Play Store kwaajili ya kudownload App hiyo.

Intruder Selfie™
Price: Free

Baada ya kupakua App hii na kuinstall vizuri kwenye simu yako unachotakiwa sasa ni kufungua app hiyo kisha fuatisha maelezo yote hapo chini.

Kwa kuanza bofya sehemu ya Grant Permision kisha bofya OK kwenye kila permision ambayo application hii inahitaji, hatua hii ni muhimu ili kufanya app hii iweze kufanya kazi vizuri.

Hatua ya pili hakikisha unabofya sehemu hii ya Grant Device Admin kisha bofya Acivate kwenye simu yako, sehemu hii ni muhimu sana kwani inasaidia mtu asiweze kuondoa app hii kwenye simu yako hadi pale utakapo taka wewe mwenyewe. Pia usisahau kuweka tiki kwenye kichumba kilicho andikwa I understand.

Baada ya hapo ingia kwa kutumia akaunti yako ya Google, Hatua hii ni muhimu sana kama unataka kutumia app hii pale simu yako inapo potea au kuibiwa, Sehemu hii itakusaidia kuweza kupata picha ya mtu aliyechukua simu yako moja kwa moja na utaweza kuipata kupitia Google Photo.

Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye app hiyo sasa utaweza kuona Menu yenye vimikato vitatu juu upande wa kushoto bofya hapo kisha bofya sehemu ya Settings.

Baada ya kubofya Setting utapelekwa kwenye uwanja wenye mipangilio mbalimbali kwaajili ya App hii, unachotakiwa kufanya ni Kuchagua Number of Picture, hii ikiwa na maana idadi ya picha zitazochuliwa na App hiyo pale mtu atakapo shika simu yako, unaweza kubadilisha na kuweka picha 2 kulingana na pendekezo lako.

Pia chini ya sehemu hiyo utaona sehemu nyingine iliyo andikwa Detection Behavior, ni muhimu kwani inasaidia kuweza kuseti app hii iweze kupiga picha baada ya kitendo gani, yaani pale mtu atakapo washa kioo cha simu yako au pale mtu atakapo kosea password kwenye simu yako. Unaweza kuchagua sehemu ya Always kama unataka picha ichukuliwe pale kioo kinapowashwa yani kwa mfano unapokuwa umeweka simu yako chini, na pia unaweza kuchagua Fail pale mtu anapokosea kuweka password kwenye simu yako.

Basi kwa kufanya hatua hizi basi utakuwa umeweka ulinzi kwenye simu yako na kila mara utakapo kuwa umeweka mahali simu yako pale mtu atakapo ishika basi mtu huyo ataweza kupigwa picha moja kwa moja bila yeye kujua na utaweza kuikuta picha hiyo ndani ya App hiyo pale tu unapo ifungua. Na kama simu yako imeibiwa basi picha ya mtu huyo aliye iba unaweza kuikuta kwenye tovuti au App ya Google Photo ambayo inakuwa kwenye kila akaunti ya Gmail.

Njia hii ni nzuri sana Guys na ukweli inasaidia pale mtu anaposhika simu yako bila wewe kujua, na kwa wale wenye wapenzi wenye wivu kupitiliza nadhani hii itakufaa sana pale unapokuwa umelala alafu mtu anashika simu yako bila hata wewe kujua… hahahha.. anyway natumaini maujanja haya yatakusaidia kwa namna moja au nyingine kama umekwamba usiache kutuambia kupitia maoni hapo chini au kupitia tovuti ya Tanzania Tech Forums.

8 comments
  1. Sasa hii app ya intruder selfie nikitaka ika upload kwenye google drive automatic si inatakiwa uwe na Mb pia data iwe on sasa kama Simu yangu haina Mb nitamjuaje aliyeniibia Simu pia picha ku upload bila data kuwa on inawezekanaje?

  2. Kama hauna mb cm ikipotea utamfaham vipi tayale ixhaibiwa maana bila kuwasha dart muda wote uwez kufanikisha zoezi msaada kwailo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use