Njia za Kufuata Kununua Simu Kupitia Maduka ya Kariakoo

Fuata njia hizi ili uweze kununua simu bora kupitia soko la kariakoo
Kununua Simu Kariakoo Kununua Simu Kariakoo

Najua utakua umeshangaa kichwa cha habari lakini naomba uchukue nafasi yako kusoma makala hii na utajua ni kwanini nimeamua kuiandika, pia njia hii itawahusu wale ambao ni wageni na pia itawahusu wale ambao ni wazoefu na uhakika kwa namna moja ama nyingine lazima utapata chochote kupitia hapa.

Mambo yafuatayo ndio mambo muhimu ambayo ningependa kushiriki na wewe ili uweze kuyajua na kuchukua hatua pale unapoamua kwenda kununua simu kupitia maduka ya simu Kariakoo. Kuzingatia hayo twende basi tukafundishane hatua hizi muhimu sana kwa wakazi wa Dar es salaam na hata wale ambo wanapenda kuja Dar es salaam kununua simu.

1. Fanya Utafiti Kabla ya Kwenda Kariakoo Kununua Simu

Ni vyema sana kuwa makini kabla ya kwenda Kariakoo hasa kununua simu, hii ni kutokana na Kariakoo ni sehemu ya wauzaji wenye tabia tofauti hivyo ni muhimu kujiandaa kwa kufanya utafiti wa bidhaa au simu unayotaka kabla ya kwenda kununua simu hio. Unaweza kuanza kwa kufanya utafiti mtandaoni kujua sifa za simu ikiwa pamoja na njia rahisi za kutofautisha simu halisi na feki, yote hayo unaweza kuyapata kwa kutafuta kwenye Google au kupitia mtandao wa YouTube.

Advertisement

2. Siku Nzuri ya Kwenda Kariakoo Kununua Simu

Kwanza ningependa nikuweke wazi kuwa, soko la Kariakoo ni moja kati ya soko linalo tegemewa sana na watu wote na hasa wanunuzi wa vifaa vya kieletroniki kama simu na vitu vingine. Kuzingatia hayo hapa nependa nikushauri siku bora ya kwenda Kariakoo kununua simu ni siku za wiki yani hapa nazungumzia Jumatatu mpaka Alhamisi.

Sababu ni nyepesi tu, watu wengi huenda Kariakoo siku za mwisho wa wiki hii ni kutokana na watu wengi hata waliojiriwa kupata nafasi ya kwenda Kariakoo kipindI hicho hivyo kufanya soko la Kariakoo kufurika. Na hii inakuwa ni tatizo sababu wakati unanunua simu hupati hata muda wa kuongea na muuzaji kwa sababu anakuwa na wateja wengi na pia hii kufanya bei kuwa kubwa au muuzaji kuwa na msimamo wa bei kutokana na kuwa na wateja wengi. Binafsi ningependa nikushauri kwenda Kariakoo siku ya jumatatu.

3. Hakikisha Unamuda wa Kutosha

Hapa naongea na wale wazoefu pamoja na wageni, Mara nyingi watu wazoefu wa kwenda kununua simu Kariakoo au hata wale wageni wanakosa nafasi ya kupata vitu vizuri kwa bei nafuu kutokana na tabia ya kwenda sehemu moja. Hii hufanya anaye uza bidhaa kubaki na bei hiyo hiyo hata kama kitu anacho uza kwa sasa kimeshuka bei, inaweza ikawa faida kununua simu kwa mtu mmoja kwa sababu ya uaminifu na vitu vingine kama hivyo, lakini pia nivizuri kuhakikisha unatembelea maduka mbalimbali ili kuangalia utofauti wa bei za simu pamoja na ubora sambamba na muundao wa simu unayotaka kununua ikiwa pamoja na muda wa kukagua simu vizuri.

4. Hakikisha Unapewa Box la Simu Unayonunua

Kingine cha muhimu unapoenda kununua simu Kariakoo ni kuwa, mara nyingi wauzaji wa simu hasa wa Kariakoo hupenda kuuza simu bila box au wakati mwingine kutoa simu na box ambalo ni tofauti. Ni vyema kuahakikisha unapewa box halisi sababu hii husaidia pale unapo poteza simu yako. Kwenye box la simu yako kuna vitu muhimu sana kama IMEI Namba ambayo hii huwa muhimu sana pale unapotaka kuipata simu yako. Pia box hua kama risiti ya pili kudhibitisha kuwa wewe ndie mmiliki halisi wa simu hiyo.

5. Beba Begi kwa Wanaume au Mkoba kwa Wanawake

Hakikisha unapoenda Kariakoo kununua Simu, beba begi au mkoba kwani hii itakusaidia kuweka simu yako mahali salama. Kama nilivosema awali Kariakoo ni soko la watu wengi na kama unavyojua soko kuna watu wengi wa kila aina hivyo ni muhimu kubeba mkoba ambao utaweza kuweka simu yako kwa ulinzi zaidi.

6. Hakikisha Unafanya Mapatano Pale Unapotaka Kununua

Ukweli ni kuwa kila muuzaji wa simu huwa na tabia ya kuongeza bei kwani kila mtu anapenda kupata faida pale anapouza bidhaa flani, Hivyo basi nilazima kuhakikisha unafanya mapatano kwa muda kidogo kabla ya kununua hii husaidia kwani muuzaji ushuka bei baada ya kuona kwamba umefanya mapatano kwa muda mrefu, Niamini utashangaa bei inavyoshuka kuliko ambavyo ungedhani..!

7. Usinunue Simu Iliyotumika Kariakoo

Kitu ambacho naweza kukwambia, Mara nyingi watu wakienda Kariakoo kununua simu ubadilisha mawazo tu kutokana na kuona simu iliyotumika ya bei rahisi na hivyo kujikuta wananunua simu na kuachana na ile simu ya lengo ambayo ndio ilikupeleka Kariakoo. Ukweli ni kwamba ni watu wa chache sana uamua kuuza simu kwa lengo zuri na ni watu wengi sana uamua kuuza simu kutokana na sababu za ubovu wa simu hivyo hakikisha mtu akutoi kwenye lengo lako. Waswahili walisema “Usiache Mbachao kwa msala Upitao”.

8. Hakikisha Unapewa Warranty na Risiti

Kitu cha mwisho ambacho ningependa ukiweke akilini ni kuwa hakikisha sana sana unapewa risiti pamoja na warranty ya simu kwani hii itakusaidia sana pale simu itakapo haribika kwa miezi ya mwanzo na itakusaidia sana pale unapokutana na dhahama yoyote Kariakoo. Pia hakikisha risiti unaiweka mfukoni tofauti na simu kwani hii itakuwa muhimu pale inapotokea umeibiwa simu hiyo hapo hapo sokoni Kariakoo.

Na hizo ndio njia mbazo najua zinaweza kukusaidia wew kupata simu nzuri na bora pale unapo kwenda kununua simu Kariakoo, Njia hizi sio pekee ambazo zitaweza kukusaidia zipo njia nyingi sana na kuna watu ambao ni wazoefu zaidi wanaoweza kukusaidia. Kama una maswali au unakitu cha kuongeza unaweza kuandika kwenye maoni hapo chni na tutaongeza hatua hizi hapo juu.

1 comments
  1. naoma kuuliza njia rahis ya kujumua mzigo wa sim za mkononi kutoka china kuja Tanzania mim ni mfanya biashara ndo naanza

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use