Jaribu Apps Hizi Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android (2020)

Hizi hapa apps nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako
Jaribu Apps Hizi Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android (2020) Jaribu Apps Hizi Nzuri Kwenye Simu Yako ya Android (2020)

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android basi lazima unajua kuwa tumekuwa tukiandika makala kuhusu app nzuri za Android ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako. Makala hii sio ya tofauti kwani hapa pia tumekuletea app nyingine nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako ya Android.

Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi twende kwenye app hizi, kumbuka unaweza kupakua app husika kwa kubofya jina la app au kupitia link itayo tajwa kwenye maelezo.

Kama wewe ni kama mimi na umekuwa ukisahau kusoma notification mbalimbali kwenye simu yako basi app hii ya FilterBox ni app nzuri sana kwako. App hii inakuja na uwezo wa kuweka kumbukumbu ya Notification zako zote, huku ikikupa uwezo wa kuona ni app gani inayo tuma notification zaidi pamoja na mambo mengine mengi.

Advertisement

Big File Cleaner
Price: Free

Kama simu yako imekuwa ikijaa haraka bila kujua uhifadhi wa simu yako umetumika kwenye nini basi basi app hii ya Big File Cleaner ni app nzuri sana kwako. App hii itakupa uwezo wa kujua mafile makubwa yaliyo jificha kweye simu yako ikiwa pamoja na kukupa uwezo wa kuyafuta na kuongeza uwezo zaidi wa simu yako.

Pinnit
Price: Free

Kama umekuwa ukisahau sana mambo mengine lakini umekuwa ukikumbuka kusoma meseji zako basi pengine app hii inaweza kusaidia uwe unakumbuka kila kitu. Pinnit ni app ambayo itakusaidia kuweka kumbukumbu ya mambo yako kwa kuandika ndani ya app hii, na app hii itaweka kumbukumbu hizo kwenye sehemu ya juu ya notification na utakuwa unaona ujumbe huo kila mara unapofungua sehemu ya Notification.

Kama umekuwa ni mtu wa kurekodi sauti mara kwa mara kwa kutumia simu yako pengine ni wakati wa kujaribu app hii mpya kutoka Dolby. App hii inakupa uwezo wa kurekodi sauti vizuri ikiwa pamoja na uwezo wa kuchuja sauti hata kama umerekodi sauti kwenye sehemu yenye kelele.

Kama wewe ni mpenzi wa simu yako sana na ungependa kubadilisha muonekano wa simu yako mara kwa mara basi jaribu app hii ya TruePick’s. App hii inakuja na wallpaper nzuri sana ikiwa pamoja na mambo mengine mengi ya kubadilisha simu yako na kuwa na muonekano mzuri.

Copy Text On Screen
Price: Free

Kama umekuwa ukipata shida kunakili maandishi ambayo yapo kwenye picha basi usijali.. app hii ya Copy Text On Screen ni app nzuri ambayo itakusaidia kunakili maandishi yote yaliyopo kwenye picha yoyote. Unacho takiwa kufanya ni ku-screenshot na kisha share na app hii kisha utaweza kunakili maandishi yote yaliyopo kwenye picha.

Tangi Quick Videos
Price: Free

Tangi ni app mpya kutoka Google, app hii inakuja na mfumo ambao utakusaidia kuangalia video fupi zenye kukupa elimu kwa haraka. App hii ni mpya kutoka kampuni ya Google na inapatikana pia kupitia kwenye tovuti hapa.

Kama unaona siku yako imeharibika au una mawazo kwa namna yoyote basi unaweza kujaribu app ya cheka point, app hii inakupa uwezo wa kuangalia na kupakua video za kuchekesha moja kwa moja kwenye simu yako. App hii inapakiwa vichekesho kila siku hivyo utapata vichekesho vipya kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Na hizo ndio app nzuri ambazo unaweza kujaribu kwenye simu yako ya Android, kama unataka kujua app nyingine nzuri unaweza kusoma hapa kujua app ambazo ni mbadala wa soko la Play Store. Endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

1 comments
  1. Kuna app moja kwa wale wasiojua kiingerez inaitw TRANIT itawasaidia kutrenslate sehem yeyot kwenye mitandao ni inzuri sana

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use