Kampuni ya Apple Yazindua Mfumo Mpya wa iOS 13

Mfumo huu mpya unakuja na sehemu mpya ya Dark Mode
Kampuni ya Apple Yazindua Mfumo Mpya wa iOS 13 Kampuni ya Apple Yazindua Mfumo Mpya wa iOS 13

Mkutano wa WWDC 2019 tayari umeanza rasmi na kampuni ya Apple imesha zindua mfumo mpya wa iOS 13, kwa mujibu wa Apple mfumo huu ni moja kati ya mfumo bora zaidi wa iOS na pia ni mfumo ambao umefanyiwa maboresho zaidi kuliko mifumo yote ya iOS.

Kupitia makala hii tutenda kungalia kila kitu ambacho kimetangazwa kinacho husika na mfumo huu mpya wa iOS 13, hivyo nakushauri usome makala hii hadi mwisho kwani yapo mambo mengi ya muhimu ambayo tutaongelea kwenye makala hii ambayo ni muhimu kufahamu kwa wewe mtumiaji wa simu au kifaa kinacho tumia mfumo wa iOS.

Muonekano wa Giza (Dark Mode)

Muonekano wa giza umekuwa ni kitu cha muhimu kwenye programu za siku hizi ndio maana kampuni ya Apple imetangaza kuleta sehemu ya Dark Mode ndani ya mfumo wa iOS 13.

Advertisement

Kwa mujibu wa Apple, kila app inayokuja ndani ya mfumo wa iOS 13 itakuwa inafanya kazi na mfumo wa huo wa Dark Mode, na hata pia sehemu ya Notification inasemekana itakuwa inaweza kufanya kazi vizuri kwa kubadilika muonekano na kuwa na muonekano wa giza.

Keyboard Mpya (Quick Path)

Apple imefanya maboresho kiasi kwenye keyboard yake na sasa imeongeza aina mpya ya kutumia keyboard hiyo. Kwa mujibu wa Apple sasa utaweza kutumia keyboard hiyo kwa kutumia njia mpya inayoitwa “Quick Path” . Njia hii itakusaidia kuandika kwa kupapasa swipe juu ya namba na herufi kama ilivyo kwenye apps kama vile SwiftKey, Swype, au Gboard.

Kampuni ya Apple Yazindua Mfumo Mpya wa iOS 13

App ya Kukumbusha (Reminder)

App ya Reminder imefanyiwa maboresho kadhaa kwa kuongezewa vipengele kama vile “Today,” “Scheduled,” “Flagged,” pamoja na “All”. Vipengele hivi vinaweza kufanya kutumia kwa urahisi app hiyo ya kukumbusha.

Mabadiliko ya App za Mail, Notes na Safari

Kwa upande mwingine apple imebadilisha baadhi ya sehemu kwenye app zake za Mail, Notes na Safari. Mail inakuja na sehemu mpya ya desktop formatting, App ya Notes inakuja na sehemu mpya gallery view ambayo itakusaidia kuona Notes zako zote kwenye ukurasa mmoja. Kwa upande wa app ya Safari yenyewe itawekewa sehemu mpya ya per-website preferences ambayo itakusaidia kutembelea tovuti mbalimbali kulingana na uchaguzi wako wa muonekano.

Mabadiliko App ya Ramani (Apple Maps)

Kwa upande wa app ya ramani, Apple imetangaza kufanya mabadiliko ya ndani ya app hiyo na pia imeongeza sehemu mpya ya kuona ramani za miji (Street View). Kwa mujibu wa Apple sehemu hiyo inasemekana kuja kwa baadhi ya miji ya nchini marekani mwishoni mwa mwaka 2019.

Kampuni ya Apple Yazindua Mfumo Mpya wa iOS 13

Mabadiliko ya Ulinzi (Privacy)

Kwa upande mwingine Apple imetangaza kuwa mfumo huu utakuwa una angalia zaidi kwa upande wa ulinzi au Privacy. Apple imeongeza aina mpya ya ulinzi ambao sasa utaweza kuzuia app yoyote kutumia sehemu ya Location mara moja tu, yaani pale unapo ruhusu app kutumia sehemu ya location haitoweza kuendelea kutumia sehemu hiyo mpaka itakapo omba tena kutumia sehemu hiyo. Hii itasaidia sana kwa apps ambazo zinamtindo wa kutumia location bila wewe kujua.

Pia Apple inakuja na sehemu mpya ya “Sign in with Apple” sehemu hii ni kama ile ya Sign with Google ambayo pia inakupa uwezo wa kutengeneza akaunti kwenye apps mbalimbali na tovuti bila kuweka password na username, sehemu hii pia itakuja kwa wabunifu wa programu (developers).

Mabadiliko ya Katuni za Memoji

Apple pia imatangaza mabadiliko machache ya memoji ambapo sasa utaweza kutengeneza memoji kwa kutumia aina mpya ya sehemu ambazo zitapatikana ndani ya app hiyo. Pia utaweza kutumia memoji kama sticker ndani ya programu ya iMessenger.

Picha za Wasifu Kwenye iMessenger

Kwa mujibu wa Apple sasa utaweza kuweka picha yako ya wasifu kwenye iMessenger kama ilivyo kwenye programu ya WhatsApp. Utaweza kushiriki na wengine picha na jina lako na watu wengine wataweza kuona kama inavyokuwa kwenye app ya WhatsApp, pia utaweza kutumia Memoji kama picha yako ya wasifu (Profile Picture) ndani ya App hiyo.

Sehemu Mpya za Picha na Kuedit Video

Apple pia imeongeza sehemu mpya kwenye app ya Photo pamoja na njia mpya ya kuedit video kwenye mfumo wa iOS 13. Kupitia sehemu ya video utaweza kuedit vitu mbalimbali kama brilliance, highlights, shadows, contrast, saturation, white balance, sharpness, definition, vignette, pamoja na noise reduction, yote hayo kupitia kifaa chako chenye mfumo wa iOS 13.

App ya Photo inakuja na mtindo mpya kabisa ambapo sasa app hiyo itakuwa inatumia mfumo wa AI kuweza kuondoa picha zinazo jirudia au picha za screenshot za muda mrefu ndani ya App yako ya Photo.

App Mpya ya Find My

Apple pia imetangaza kuja na app mpya ndani ya mfumo wa iOS 13, App ambayo ni mchanganyiko wa apps za Find My Friends na Find My iPhone ambazo hutumika kupata kifaa chako cha iOS pela kinapo potea. App hii mpya ya Find My itakuwa na uwezo wa kupata kifaa chako hata kama kimezimwa, app hiyo hutumia mfumo wa kisasa wa bluetooth kuweza kutuma signal na kumsaidia muhusika kuona simu yake ilipo hataka kama imezimwa data au imezimwa kabisa.

Njia mpya ya Kuingiza Mafile

Apple pia imeongeza uwezo mpya wa kutumia Flash kwenye mfumo huo wa iOS 13, kupitia app ya Files utaweza kutumia Flash na kuamisha data zako kutoka kwenye flash kuja kwenye app ya File moja kwa moja.

Simu Zitakazopata iOS 13

Mbali na yote Apple imetengaza kuwa simu zote za iPhone kuania iPhone 6S zitapata mfumo wa iOS 13, isipokuwa simu za iPhone 5S na iPhone 6. Mfumo huu unatarajiwa kuanza kutumika kwa majaribio kuanzia siku ya kesho huku toleo kamili likitarajiwa kuzinduliwa rasmi baadae mwaka huu.

Kampuni ya Apple Yazindua Mfumo Mpya wa iOS 13

Na hayo ndio yote ambayo yametangazwa kwenye ujio wa mfumo wa iOS 13, kama unataka kujua zaidi kuhusu mkutano wa WWDC 2019 hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech au tembelea ukurasa wetu wa WWDC 2019.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use