Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jiandae na Infinix NOTE 7 Hapa Nchini Tanzania (Bigi Makini)

Simu mpya ya Infinix Yenye kioo kikubwa na uwezo mkubwa
Jiandae na Infinix NOTE 7 Hapa Nchini Tanzania (Bigi Makini) Jiandae na Infinix NOTE 7 Hapa Nchini Tanzania (Bigi Makini)

Kampuni pendwa ya simu Tanzania, Infinix Mobility iko mbioni kuleta simu yenye hadhi ya juu Infinix NOTE 7 na kupewa jina la BIGI MAKINI kutokana na kioo chake kuwa na size kubwa 6.95 inch na uwezo mkubwa wa camera 48MP na processor ya G70 kutoka Mediatek.

Jiandae na Infinix NOTE 7 Hapa Nchini Tanzania (Bigi Makini)

Advertisement

Processor yenye speed ya G70 inauwezo mkubwa wenye  kuwezesha matumizi mbali mbali kwa wakati mmoja bila kuchoka, NOTE 7 inatumia OS mpya kutoka Google, Android 10. Simu hii haitazinduliwa rasmi kama utaratibu wao ulivyozoeleka lakini kupitia mitandao yao ya kijamii @infinixmobiletz wameeleza sifa na umaradufu wa simu hii. Yawezekana kuwa ndiyo simu bora zaidi ya Infinix kutoka mwaka huu.

Jiandae na Infinix NOTE 7 Hapa Nchini Tanzania (Bigi Makini)

“Vile vile tunawashukuru wa Tanzania kuipokea vyema Infinix NOTE 7 Lite, iliyoingia sokoni katika ya mwezi huu wa April. Infinix NOTE 7 ni simu inayoweza kumsaidia mfanyakazi katika shughuli zake za kila siku kwani inaweza kutunza kumbukumbu kupitia 64GB na RAM ya 4GB, pia kuna sifa nyingine kama Document Scanning ambazo huitaji kupakua app ya ziada. Tumeunganisha Teknolojia ya kisasa zaidi ili kuwanufaisha wateja wetu. Pamoja na sifa zote za simu hii, tumeweka bei ya kawaida kwa mtanzania mwenye kipato cha kati” Aisha Karupa, Afisa Mahusiano.

Jiandae na Infinix NOTE 7 Hapa Nchini Tanzania (Bigi Makini)

Tunawakaribisha wateja wetu kununua Infinix NOTE 7 Lite sasa zipo madukani, na kwa kila mteja atakayenunua atapata zawadi mbali mbali kutoka Infinix, ikiwemo, magic cup, Notebooks, Speaker vile vile unaweza kujishindia Simu nyingine ila hii itakuwa kwa wateja wa NOTE 7 pindi itakapoingia sokoni mwezi ujao.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use