Hii Ndio Simu Inayofanya Poa Kwa Sasa Sokoni

Infinix HOT 30 Helio G88
Hii Ndio Simu Inayofanya Poa Kwa Sasa Sokoni Hii Ndio Simu Inayofanya Poa Kwa Sasa Sokoni

Samsung ni moja ya brand kongwe katika soko la simu basi moja kwa moja nakuletea tofauti kati ya simu hizi mbili za daraja la kati ‘Infinix HOT 30 na Samsung A14’ kwa kuangalia features muhimu kama bei, camera, processor, resolution, video features, chajing wat, battery, design, ram na nyinginezo.

 • Processor: Infinix HOT 30 Helio G88 na Samsung A14 Helio G80.

Infinix HOT 30 kwa sasa ndio simu yenye uwezo mkubwa kwenye gaming na yenye kupatikana kwa bei nafuu kulinganisha na simu yengine za daraja la kati.

Hii Ndio Simu Inayofanya Poa Kwa Sasa Sokoni

Advertisement

 • Teknolojia ya fast chaji: Infinix HOT 30 33Wat, A14

Infinix HOT 30 inakuchukua lisaa limoja tu kwa battery ya simu yako kujaa chaji kufikia asilimia 100 lakini Samsung a14 inakuhitaji usubiri kwa masaa mawili kwa battery kufikia asilimia 100.

 • Memory ya ndani: Infinix HOT 30 8GB Ram kuongezeka hadi 16GB Ram/256GB Rom, A14 6GB Ram/128GB Rom.

Ram ya HOT 30 ni kubwa zaidi, Kadri simu yako inavyokuwa na Ram zaidi, ndivyo utendakazi wake unavyoongezeka wakati wa kubadilisha programu. Ikiwa ni mtumiaji wa programu zenye kuchukua nafasi kubwa ya memory kama kuediti video, kucheza games kupitia simu, basi unaweza yafanya haya kwa wepesi kupitia Infinix HOT 30 kwani si rahisi simu yako kugoma goma wala kupata moto. Utendaji kazi wa Ram ya HOT 30 ni hodari mara mbili zaidi kulinganisha na Ram ya Samsung a14.

 • kurecord video: Infinix HOT 30 1440@30fps, A14 1080@30fps.

Kwenye swala zima la kuchukua matukio yaliyo kwenye mwendo au kuchezesha games Infinx HOT 30 ni bora zaidi sababu fremu yake ni kubwa, hivyo hufanya mwendo wa tukio au game uonekane wa asili zaidi na usio na mawimbi ambapo kwa Samsung a14 ipo chini katika technolojia hii na huweza kukufanya usifurahie video ambazo umejaribu kurecord au kudownload na pia kuleta mikwaruzo kwenye kucheza game ya simu.

 • Uang’avu/Resolution: Infinix HOT 30 1080×2460, A14 1080×2408.

Simu zote zinaresolution nzuri isipokuwa ya Infinix HOT 30 imeongezeka uwezo zaidi kama ambavyo inaonekana hapo juu na kadiri resolution inapokuwa kubwa na ndivyo simu yako inavyoweza kuonyesha picha, videos kwa uhalisia na hata uang’avu wa kioo unapozidi kuvutia.

 • Camera kuu ya nyuma kwa simu zote mbili 50MP.
 • Battery zinalingana zote zikiwa na mAh5000.
 • Kioo: Infinix HOT 30 6.78inch, A14 6.6inch.
 • Teknolojia ya kufanya kioo kuwa laini/smooth wakati wa kuperuzi ni 90Hz kwa simu zote.

Sifa nyengine kama kamera, battery, ukubwa wa kioo na refresh rate zinalingana isipokuwa utendakazi wake unaweza pishana, Infinix HOT 30 ni bora kwa sababu ya features kama processor, resolution, video features na fast chaji vinaongeza ubora kwenye kupiga picha kuwa na rangi nzuri na zenye kung’aa, mtumiaji kuokoa muda endapo simu itaishiwa chaji kutokana na fast chaji, refreshrate kufanya kazi kwa wepesi zaidi kutoka na usaidizi wa Ram na processor.

Hii Ndio Simu Inayofanya Poa Kwa Sasa Sokoni

 • Wembamba: Infinix HOT 30 nyembamba zaidi 8.4mm, A14 9.1mm.
 • Uzito: Infinix HOT 30 haina uzito wa kukera ni gram 196, A14 nzito zaidi gram 201.

Simu zote zinaukubwa wa kioo sawa isipokuwa Infinix HOT 30 ni nyembemba zaidi kitu kinachoifanya ivutie zaidi ukishikia mkononi au kuweka kwenye mfuko wa shati.

 • Bei: Infinix HOT 30 inapatika kwa sh.420,000, inasadikika A14 kuwa sh.450,000.

Kila muuzaji na bei yake isipokuwa InfiniX HOT 30 haizidi kiasi cha sh. 420,000 na Samsung a14 haizidi kiasi cha sh. 450,000.

Kupitia tofauti hizi nadhani nitakuwa nimekusaidia kujua ni simu gani itakupendeza kununua kwa matumizi yako ya kila siku. Lakini pia ubora wa simu sio kuwa na bei kubwa ubora wa simu ni kukupa kile unachokitaka kwa bei yenye kuendana na bidhaa yenyewe.

Ofa

simu zote zinapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania. Infinix HOT 30 ikiwa na ofa ya GB96 za internet na ofa ya punguzo la bei kwa wanafunzi wa chuo.

Kwa huduma ya haraka wapigie 0745170222 au tembelea @infinixmobiletz

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use