Microsoft Yaleta Game ya Solitaire kwenye Android na iOS

Game maarufu ya karata ya solitaire kutoka microsoft sasa inapatikana kwenye mifumo ya Android pamoja na iOS
Solitaire Solitaire

Kwa watu wengi ambao wamewahi kuwa na kompyuta Solitaire sio jina geni kwani Solitaire ni game maarufu ya kompyuta ambayo ilianza tarehe 22 May mwaka 1990. Game hii imejulikana sana kwa kuwa moja kati ya game ambazo zinakuja na mfumo wa uendeshaji wa Windows.

Game hii iliyodumu kwenye mfumo huo kwa zaidi ya miaka 25 sasa kwa mara ya kwanza game hiyo inapatikana nje ya mfumo huo wa Windows hii ikiwa na maana kwa sasa game hiyo itapatikana kwenye mifumo ya Android pamoja na iOS. Hata hivyo kampuni ya Microsoft inategemea kutoa game hiyo bure kabisa ili kuongeza idadi ya watu milioni 119 walio cheza game hiyo kwenye mifumo ya Windows 8 pamoja na Windows 10.

Unaweza kuanza kucheza game hiyo ya karata kwa kudownload kwenye simu yako sasa, bofya mfumo unaotumia hapo chini ili kudownload game hiyo sasa.

Advertisement

Solitaire – Android

Solitaire – iOS

Kama umesha download na kucheza game hiyo unaweza kutoa maoni yako hapo chini ili kusaidia wengine pia unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use