Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Game Bora Zinazo Tarajiwa Kutoka Ndani ya Mwaka Huu 2017

Kaa tayari kwa game hizi bora za PS4, Xbox One, na Nintendo Switch
game bora game bora

Mwaka 2017 ndio huo umeshanza kuyoyoma kwa upande wa teknolojia ya Game zipo game nyingi sana ambazo zinatarajiwa kuja ndani ya mwaka huu 2017. Zifuatazo ni baadhi ya game hizo bora zinazotarajiwa kuja kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Nioh

Advertisement

Mfumo: PS4
Siku ya Kutoka: February 7, 2017

Game hii ni moja kati ya game ambazo zinasubiriwa sana na wapenda game kote duniani, kama wewe ni mpenzi wa game ni vyema kutafuta game hiyo pindi tu itakapo toka (imesha toka).

For Honor

Mfumo: PS4, Xbox One, PC
Siku ya Kutoka: February 14, 2017

Kama wewe ni mpenzi wa game za kupigana na mapanga game hii ni moja kati ya game nzuri sana kwa mwaka 2017, game hii kwa sasa imesha toka lakini bado haijafika kwenye sehemu nyingi za game hapa Tanzania. Unaweza kuipata game hii kwa kuinunua kwenye mtandao.

Sniper Elite 4

Mfumo: PS4, Xbox One, PC
Siku ya Kutoka: February 14, 2017

Game hii ni moja kati ya game bora sana ya vita, toka ilipotoka game hii imekua pendekezo la wapenda game kote duniani. Kwa sasa game hii imetoka sehemu ya nne ambayo inaonyesha vita vilivyotokea italia kama wewe ni mpenzi wa game utakiwi kukosa game hii.

Halo Wars 2

Mfumo: Xbox One, PC
Siku ya Kutoka: February 21, 2017

Kwa mtu ambaye anapenda game na bado ajacheza game hii basi unakosa uhondo kwani kwa sasa hii ni sehemu nyingine mpya kwenye mfululizo wa game hii bora ambayo utoweza kuacha kuicheza pale utakapo anza.

Horizon Zero Dawn

Mfumo: PS4
Siku ya Kutoka: February 28, 2017

Horizon Zero Dawn ni game ya kisasa yenye sauti nyingi za mastaa pamoja na muonekano kama wa transformer, game hii inaonekana kuwavutia watu wengi hivyo ni vyema kuitazama na kuijaribu pale utakapo ipata.

The Legend of Zelda: Breath of the Wild

Mfumo: Wii U, Switch
Siku ya Kutoka: March 3, 2017

Game hii inayoa anza kutoka mwaka huu ni moja kati ya game bora za mfumo wa Nintendo, game hii inategemewa kutoka mwezi wa tatu lakini tayari imesha kuwa gumzo pamoja na kuzungumziwa kwenye mitandao mbalimbali.

Nier: Automata

Mfumo: PS4, Xbox One, PC
Siku ya Kutoka: March 7, 2017

Game hii ni moja kati ya game ambazo pia kwa sasa zinasubiriwa kwa hamu, kama ukifanikiwa kuipata hapo ifikapo mwezi wa tatu  ni vyema kuja hapa kutuambia game hiyo ikoje.

Tom Clancy’s Ghost Recon Wildlands

Mfumo: PS4, Xbox One, PC
Siku ya Kutoka: March 7, 2017

Kwa wale wapenda game wa muda mrefu lazima watakua wanajua game hii, mwaka huu game hii inarudi na sehemu mpya ikiwa ni mwendelezo wa stori iliyoanza mwanzo wa game hii.

Star Trek Bridge Crew

Mfumo: PSVR, Vive
Siku ya Kutoka: March 14, 2017

Game hii ni moja kati ya game zenye kutumia teknolojia mpya ya VR (Virtual Reality), kucheza game hii utavaa miwani maalumu ambapo utaweza kuona kama uko ndani ya ndege ya Star Trek. Ukweli ni moja kati ya game bora lenye kutumia teknolojia bora sana.

Mass Effect: Andromeda

Mfumo: PS4, Xbox One, PC
Siku ya Kutoka: March 21, 2017

Game hii ni moja kati ya geme bora na ukweli ni kwamba watu wengi wanasubiria game hii kwa hamu sana. Ukifanikiwa kucheza game hii utoweza kuacha kuicheza kila siku.

KUMBUKA : Bado list hii inaendela…..

Na hizo ndio baadhi ya game bora ambazo zinangojewa sana kutoka kwa mwaka huu wa 2017, kwa habari zaidi za game pamoja na mambo mengine yahusuyo teknolojia download app ya Tanzania Tech ili kupata habari kwa haraka pindi zitokapo. Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia youtube ili kujifunza na kuangalia video mbalimbali zinazohusu teknolojia.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use