Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutumia Flash Kama Ufunguo wa Kompyuta Yako

flash pasword flash pasword

Ulishwahi kujiuliza inakuaje kama ukiwa na ufunguo kwaajili ya kompyuta yako yani utumie ufunguo kufungua kompyuta yako na sio password.? kama una flash drive karibu basi leo tutaenda kujifunza namna ya kutumia flash kama ufunguo wa kompyuta yako hii ni badala ya password.

Basi kwa kuanza basi ni vyema tukajua faida za kuwa na password katika flash drive, kuwa na password kwenye flash drive hii ina kusaidia hasa pale unapokuwa unasahau kwani tunakubaliana kuwa kuna wakati mtu unakua unasahau password tena kuzingatia kwa sasa karibia kila kitu kinatumia password kuanzia email mpaka simu yako ya mkononi hivyo basi ni rahisi sana kuwa na kumbukumbu ya mahali ilipo flash yako zaidi ya kukumbuka password ya kila kifaa unachotumia. Pia ni rahisi sana kutumia kwani hakuna haja ya kutafuta sehemu ya kuweka password bali unachokifanya ni kuchomeka flash yako tu basi hapo utakua umepata uwezo wa kutumia kompyuta yako kirahisi kabisa.

Advertisement

Basi tukiwa tumesha jua hayo machache moja kwa moja twende tuka jifunze namna ya kutumia flash drive kama password ya kuwasha kompyuta yako, ili uweze kufanya haya unachohitaji ni flash na internet angalau MB100 ili kuweza kupakua programu hiyo ya ku-wezesha kutumia flash kama password ya kompyuta yako.

KUMBUKA : Huna haja ya ku-format flash yako bali hakikisha flash yako ina nafasi kidogo kama MB200 hivi au zaidi

Kwa kuanza basi cha kwanza bofya link hii hapa PREDATOR kisha pakua programu ya predator na ufanye installation kwenye kompyuta yako kumbuka kompyuta yako itaendelea kuwa on endapo flash yako itakuwa imechomekwa kwenye kompyuta yako pale unapoitoa flash yako kompyuta yako huzima moja kwa moja na kuonyesha ishara ya kuwa mtumiaji hana uwezo wa kutumia kompyuta hiyo.

Basi ukisha pakua programu hiyo install kwenye kompyuta yako baada ya hapo chomeka flash yako pale programu itakapo hitaji, kisha chagua password yako  na kisha bofya save. Hapo utakuwa umefanikiwa kuweka password kwenye kompyuta yako kwa kutumia flash.

usb-key-dongle-tools-predator

Ukisha maliza vyote hivyo kama imetokea unataka ku unstall programu hii akikisha flash inakuwa imechomekwa kisha ndo uondoe programu hiyo kwenye kompyuta yako.

Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka, pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa Tanzania tech blog. Pia usisahau kubofya hako ka-LOVE hapo chini ili ku-show love..!!

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use