Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutumia Simu ya Android au iOS Kwenye Windows

Sasa jibu meseji pamoja na mambo mengine kupitia kompyuta yako
Jinsi ya Kutumia Simu ya Android au iOS Kwenye Windows Jinsi ya Kutumia Simu ya Android au iOS Kwenye Windows

Kama wewe ni mmoja wa wasomaji wa tovuti hii basi lazima utakuwa unajua kuwa tulishawahi kuongelea njia ya kutumia simu ya Android kwenye kompyuta, lakini kwa sababu ya kubadilika kwa teknolojia na uwepo wa njia nyingine bora zaidi leo nimekuletea njia bora zaidi ya kutumia simu ya Android pamoja na iOS kwenye kompyuta yako yenye Windows 10.

Kumbuka njia hii ni rahisi sana na inafanya kazi vizuri sana pengine kuliko njia zote za awali ambazo tumewahi kuzionyesha kupitia tovuti hii. Kumbuka kitu cha muhimu unahitaji kuwa na kompyuta yenye mfumo wa Windows 10, na pia kama kompyuta yako ni aina ya Dell, basi njia hii ni rahisi zaidi kuliko wale ambao wanatumia kompyuta ambazo sio za Dell, lakini pamoja na hayo njia hii inafanya kazi kwenye kompyuta zote zenye Windows 10.

Advertisement

Kabla ya kuendelea hebu chukua muda mfupi kuangalia jinsi njia hii inavyofanya kazi kupitia kwenye video hapo chini. Kama hichi ndio kitu ambacho unahitaji basi nakukaribisha kuendelea kusoma makala hii hapo chini.

Kama nilivyo kwambia, kupitia njia hii utaweza kufanya mambo mengi sana kama ulivyoweza kuona kwenye video hapo juu. Kumbuka kama unatumia kompyuta ya Dell basi njia hii ni rahisi zaidi kwako, ila pia kama unatumia kompyuta nyingine yoyote yenye Windows10 basi usijali kwani nitakuwa na wewe hatua kwa hatua.

Kwa kuanza kama unatumia kompyuta ya Dell ya kuanzia mwaka 2018 na kuendelea basi huna haja ya kufanya hatua hapo chini bali kitu unacho takiwa kufanya ni kupakua App ya Dell Mobile Connect kupitia link hapo chini.

Kama unatumia kompyuta nyingine yoyote yenye mfumo wa Windows 10 au kompyuta ya Dell ilyotoka nyuma ya mwaka 2018, basi hakikisha unafuata hatua hapo chini moja baada ya nyingine.

Kupitia kompyuta yako yenye mfumo wa Windows 10, ingia kwenye sehemu ya Settings kisha bofya sehemu ya Update & Security, kisha chagua For Developer, washa sehemu hiyo kwenye kompyuta yako. Sehemu hii itakusaidia kuweza kupakua app za Windows 10 bila kupitia kwenye soko la Windows Store. Baada ya kuwasha sehemu hii basi endelea kwenye hatua inayofuata.

Pakua app ya Dell Mobile Connect hapa, baada ya kupakua app hiyo, fungua app hiyo na moja kwa moja utaweza kuona app hiyo ikianza ku-install kwenye kompyuta yako. Baada ya hapo pakua driver za programu hiyo kupitia link hapa, kisha install driver hizo na restart kompyuta yako na endelea kwenye hatua zinazofuata hapo chini.

Baada ya hapo kama unataka kutumia simu ya Android kwenye kompyuta yako basi download app ya Android hapo chini. Pia kama unataka kutumia simu ya iPhone kwenye kompyuta yako ya Windows basi pakua app ya mfumo wa iOS kupitia link hapo chini.

Dell Mobile Connect – Android

Dell Mobile Connect – iOS

Baada ya ku-install app kwenye simu yako sasa moja kwa moja fungua app ya Dell Mobile Connect kupitia kompyuta yako na fuata maelekezo yanayo onekana kwenye programu hiyo. Kitu cha msingi washa bluetooth kwenye kompyuta yako pia washa Bluetooth kwenye simu yako kisha endelea kwa kuchagua mfumo unatotumia kwenye programu hiyo kwenye kompyuta yako.

Jinsi ya Kutumia Simu ya Android au iOS Kwenye Windows

Baada ya hapo fungua app ya Dell Mobile Connect kwenye simu yako kisha bofya Pair kisha kwenye kompyuta yako bofya Next utaletewa sehemu ya kuwaka code ambazo zitakuwa zinaonekana kwenye simu yako.

Jinsi ya Kutumia Simu ya Android au iOS Kwenye Windows

Baada ya kuweka code hizo bofya Next na moja kwa moja utaweza kuona simu yako imeunganishwa na kompyuta yako moja kwa moja. Kumbuka unaweza kutumia simu yako kwenye kompyuta kufanya mambo mbalimbali kama kujibu meseji kutumia baadhi ya app na mambo mengine mengi sana kama ulivyoweza kuona kwenye video hapo juu.

Njia hii ni rahisi na ni njia ambayo binafsi naitumia kwa muda mrefu sana na nimetokea kuipenda sana kwani inanisaidia kwa sababu mara nyingi natumia kompyuta kufanya mambo mbalimbali. Kama umependa njia hii hakikisha unatembelea channel yetu ya YouTube hapa, kwani huko tunajifunza mambo mengi sana kwa vitendo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use