Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Utaweza kupakua video na audio yoyote inayopatika kwenye mtandao wa YouTube
Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Telegram ni moja kati ya programu bora sana hasa ukijua jinsi ya kutumia, programu hii inakuja na mambo mengi sana kiasi kwamba hakuna hajuae kila kitu kwani kila siku mambo yanabadilika kupitia programu hiyo.

Kwenye siku za karibuni kupitia hapa Tanzania tech tutakuwa tukiangalia njia mbalimbali za kutumia programu hii ya Telegram, njia ambazo natumaini zitakuwa na faida kwenu wote kwa namna moja ama nyingine.

Kwa kuanza siku ya leo nitaenda kuonyesha njia rahisi sana ambayo unaweza kutumia kudownload video na audio yoyote kutoka mtandao wa YouTube. Njia hii ni rahisi sana na mtu yoyote mwenye programu ya telegram anaweza kufanya hatua hizi.

Advertisement

Basi bila kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye hatua hizi, muhimu ni kuhakikisha unayo internet kwenye simu yako. Kwa kuanza hakikisha unayo programu ya telegram kwenye simu yako, na moja kwa moja bofya link hapo chini na utapelekwa kwenye ukurasa maalum ya telegram.

Bofya Hapa Telegram

Kama utapelekwa kwenye profile moja kwa moja bofya sehemu ya kuchat kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Baada ya hapo bofya Start inayopatikana chini mwisho kwenye ukurasa huo.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Baada ya kubofya Start utaweza kuona ujumbe ambao ukikuelekeza jinsi ambavyo utaweza kudownload video na audio kutoka YouTube kwa urahisi.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Unachotakiwa kufanya ni kuandika neno @vid kwenye sehemu ya kuchati, kisha acha nafasi na moja kwa moja anza kuandika jina la nyimbo au msanii unaye taka kudownload video zake.

Kwa mfano kama unataka kudownload video na audio za harmonize, utaandika kwenye sehemu ya kuchat @vid harmonize kisha utaweza kuona video mpya za harmonize zikionekana kwa juu ya sehemu ya kuchat kama unavyoweza kuona picha hapo chini.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Chagua video unayo itaka kwa kubofya jina la video, baada ya hapa subiri kwa sekunde kadhaa kisha utaweza kuona mafile yenye size tofauti yakitokea, moja kwa moja chagua format unayotaka. Kama ni video chagua sehemu ya video, au kama ni audio unaweza kuchagua MP3, M4A au OGG.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Kupata matokeo mazuri bofya link za 1080p kama unataka video zinazoonyesha vizuri, na kama unataka audio au MP3 inayo sikika vizuri basi unaweza kuchagua link zenye neno best kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Kumbuka, kuna wakati mwingine baadhi ya link hizo zinakuwa hazifanyikazi hivyo ni muhimu kujaribu link nyingine zinazopatikana kwenye ukurasa huo, baada ya kubofya link inayo fanya kazi basi utaweza kuona video au audio pakiwa baada ya kumaliza utaweza kuiona kwenye sehemu ya kuchat, moja kwa moja bofya kuweza kudownload.

Download Audio na Video za YouTube Kupitia Telegram

Baada ya hapo unaweza kupata video au audio kupitia simu yako moja kwa moja, hadi hapo utakuwa umeweza kudownload video na audio kupita app ya telegram. Kumbuka hii ni awamu ya kwanza ya mafunzo haya ya telegram, kupata mafunzo zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Kama unataka kujifunza jinsi ya kutumia kwa ukamilifu app ya telegram, basi unaweza kusoma hapa makala yetu iliyopita yenye mambo ambayo huwenda ulikuwa hujui kuhusu telegram.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use