Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Zifahamu hizi hapa channel unazoweza kuzifurahia hapa Tanzania
Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

YouTube ni moja kati ya mtandao muhimu sana kwenye ulimwengu wa sasa, watu wengi hutumia mtandao huo kupata habari, kujifunza ujuzi mpya pamoja na mambo mengine mengi. Lakini kutoka na ukubwa wa mtandao huu ni wazi kuwa kuna channel nyingi za kitanzania ambazo ukweli zina mchango mkubwa sana kujenga jamii ya kila siku ya kitanzania.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha channel ambazo huwenda ulikuwa uzijui na ambazo zina mchango mkubwa kwa maisha ya watanzania kwa namna moja ama nyingine. Kupitia makala hii hutoweza kuona channel maarufu kama millardayo au nyingine kama hizo, bali hapa utaweza kuona channel ambazo pengine watu wengi walikuwa hawazijui kabla.

Joel Nanauka

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Advertisement

Kama unataka kujifunza kuhusu nidhamu ya pesa pamoja na utajiri basi hakikisha unatembelea channel ya Joel Nanauka. Channel hii imekuwa ni chanzo cha maarifa kwangu kwa muda mrefu na ukweli kabisa Joel Nanauka ni mmoja kati ya channel bora zenye kuelimisha.

Newzfid

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Newzfid ni channel nyingine ambayo unaweza kufurahia, channel hii inakupa habari za mambo ambayo ulikuwa huyajui kuhusu vitu mbalimbali. Unaweza kujifinza kuhusu utajiri wa watu maarufu, teknolojia, na mambo mengine mbalimbali.

Richstar

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Kama unataka kujifunza ubunifu wa michoro (Graphics Design) pamoja na njia mbalimbali awali za kutengeneza muziki ikiwa pamoja na maswala mbalimbali ya teknolojia basi hakikisha unatembelea channel hii ya Richstar kwani utajifunza mambo mengi sana.

SirJeff Dennis

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Siku za karibuni binafsi nimekua nikijifunza maswala ya forex na ndipo nilikutana na channel hii ya SirJeff Dennis. Channel hii inatoa ushauri wa maswala ya fedha na ukweli inaonyesha kuwa channel hii itakuwa maarufu sana siku za karibuni. Kama unategemea kujifunza kuhusu maswala ya fedha hasa Forex basi unaweza kutembelea channel hii.

Swahili Fairy Tales

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Kama unao watoto wanaopenda simulizi nzuri za hadithi basi na uhakika watapenda sana channel hii, ukweli ni kwamba hadithi hizi zinaweza kuvutia hata watu wazima na kizuri ni kwamba hadithi hizi zina hadithiwa kwa lugha ya kiswahili. Jaribu kuangalia channel hii kisha utaniambia.

YIB

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Kama wewe ni mpenzi wa channel za simulizi basi pengine unaweza kujarbu kuangalia channel hii, channel hii inakuja na simulizi mbalimbali za kusisimu ambazo zinahusisha mambo mbalimbali ambayo tayari yalisha tokea kipindi cha nyuma, stori hizi zinaweza kuwa zinatisha huku zikielimisha au kuburudisha.

Mapishi Rahisi

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Kama lilivyo jina la channel hii, utaweza kujifunza mapishi rahisi ya kisasa. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kujifunza kupika chakula cha kisasa na kupika kwa ufanisi wa hali ya juu basi hakikisha unafuatilia channel hii kwani ukweli utajifunza mambo mengi sana ya mapishi.

Changamkia Fursa

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Kama unataka kujifunza ufugaji bora wa kuku basi hakikisha unafuata channel hii ya Changamkia Fursa. Channel hii inatoa elimu ya ufugaji bora wa kuku ikiwa na hatia za jinsi ya kuanza ufugaji pamoja na mambo mengine mengi kuhusu ufugaji wa kuku kwa ujumla.

YahStoneTown

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Kama unataka kujua stori za watu maarufu hapa nchini Tanzania basi nakushauri ufuatilia channel hii ya YahStoneTown. Channel hii ambayo inaongozwa na mtangazaji maarufu wa kipindi cha mkasi (Salama) inaweza kuwa ni moja kati ya channel bora sana kwa sasa hasa pale unapotaka kujua stori za watu maarufu hapa nchini Tanzania.

Swahili Universe

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Kama wewe ni mpenzi wa filamu za kiswahili kutoka hapa Tanzania basi pengine unaweza kujaribu kuangalia channel hii ya Swahili Universe. Channel hii inakuja na filamu mbalimbali za kitanzania ambazo unaweza kuangali moja kwa moja kupitia mtandao wa YouTube. Kama wewe ni mpenzi wa bongo movie basi angalia channel hii.

Tanzania Tech

Channel Nzuri za Watanzania Kupitia Mtandao wa YouTube

Ingawa watu wengi hapa mnaifahamu lakini sio vibaya kama niki wafahamisha wale ambao hawajui kuhusu channel yetu. Kupitia channel yetu utaweza kujufunza mambo mbalimbali yahusuyo teknolojia ikiwa pamoja na kufahamu njia mbalimbali za kutengeneza pesa mtandaoni.

List inaendelea..

Kwa sasa hizi ndio baadhi ya channel ambazo unaweza kuzifuatili kwa hapa nchini Tanzania, unaweza kuendelea kutembelea makala hii ili kujua pale tutakapo ongeza channel zaidi ikiwa pamoja na kuondoa channel nyingine ambazo zimekuwa maarufu zaidi baada ya kufahamika.

Kama unafahamu channel nyingine nzuri unaweza kushare jina la channel kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutaongeza channel hiyo kwenye list hii.

3 comments
  1. Hile habari ya Diamond kufikisha views bilioni moja youtube amkuandika amekuwa msanii kwa kwanza chini ya jangwa la sahara kufikisha B1views. Hii ndo hina humuhim zaidi kuliko hile

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use