Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Hii hapa list ya watu wanaolipwa pesa nyingi kupost Tangazo kwenye mtandao wa Instagram
Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020) Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi najua unajua kuwa tulishawahi kuletea list ya watu wanaolipwa pesa nyingi kupost tangazo kwenye akaunti zao za mtandao wa Instagram kwa mwaka 2018, hivi leo nimekuletea list hii kwa mwaka 2020 kwa mujibu wa tovuti ya hopperhq.

Bila kuendelea kupoteza muda zaidi basi karibu ufahamu list ya watu hawa mashuhuri wanaolipwa pesa nyingi kuposti tangazo kuliko watu wengine duniani.

20. Rihanna

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Advertisement

Analipwa Dollar $449,000 sawa na TZS Bilioni 1.04 kwa Posti Moja.

Robyn Fenty, ambae pia anajulikana kwa jina lake la Rihanna, ni mwanamuziki, mwigizaji wa Marekani, mtayarishaji, na mfanyabiashara.

19. Demi Lovato

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $455,000 sawa na TZS Bilioni 1.05 kwa Posti Moja.

Demetria Devonne Lovato ni mwanamuziki, mwigizaji wa Marekani, mtayarishaji, na mfanyabiashara.

18. Kevin Hart

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $499,000 sawa na TZS Bilioni 1.15 kwa Posti Moja.

Kevin Darnell Hart ni mchekeshaji wa kwenye majukwa (Stand-up Comedy), muigizaji, mtayarishaji pamoja na mfanyabiashara kutoka Philadelphia, Pennsylvania, nchini Marekani.

17. Kourtney Kardashian

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $514,000 sawa na TZS Bilioni 1.19 kwa Posti Moja.

Kourtney Mary Kardashian ni ndugu wa mwana mitindo, socialite, mfanyabiashara pamoja na muigizaji Kim Kardashian. Kourtney Mary Kardashian nae ni mwana mitindo, socialite, mfanyabiashara pamoja na muigizaji.

16. Miley Cyrus

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $593,000 sawa na TZS Bilioni 1.37 kwa Posti Moja.

Miley Ray Cyrus ni mwanamuziki, mwigizaji wa Marekani, mtayarishaji, na mfanyabiashara.

15. Khloe Kardashian

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $608,000 sawa na TZS Bilioni 1.40 kwa Posti Moja.

Khloé Alexandra Kardashian ni mwana televisheni wa Marekani,sociallite, mfanyabiashara, na mjasiriamali.

14. Kendal Jenner

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $608,000 sawa na TZS Bilioni 1.40 kwa Posti Moja.

Kendal Jenner ni mwana televisheni wa Marekani, mwanamitindo, socialite, na mfanyabiashara. Kendal Jenner ni ndugu wa Kylie Jenner.

13. Nicki Minaj

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $625,000 sawa na TZS Bilioni 1.44 kwa Posti Moja.

Onika Tanya Maraj-Petty ni mwanamuziki, mwigizaji wa Marekani, mtayarishaji, na mfanyabiashara.

12. Jennifer Lopez

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $663,000 sawa na TZS Bilioni 1.53 kwa Posti Moja.

Jennifer Lynn Lopez au J-Lo ni Mwigizaji wa Amerika, mwimbaji, mcheza muziki, mbuni wa mitindo, mtayarishaji, na mfanyabiashara.

11. Lionel Messi

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $695,000 sawa na TZS Bilioni 1.61 kwa Posti Moja.

Lionel Andrés Messi Cuccittini ni mchezaji wa soka wa Argentina ambaye anacheza kama mchezaji wa mbele wa klabu ya Hispania Barcelona na timu ya taifa ya Argentina.

10. Neymar da Silva Santos Junior

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $704,000 sawa na TZS Bilioni 1.63 kwa Posti Moja.

Neymar da Silva Santos Junior ni mchezaji wa soka wa Brazil ambaye anacheza kama mchezaji wa mbele wa klabu ya Kifaransa Paris Saint-Germain na timu ya taifa ya Brazil.

9. Taylor Swift

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $722,000 sawa na TZS Bilioni 1.67 kwa Posti Moja.

Taylor Alison Swift ni mwandishi wa nymbo-mwimbaji wa Amerika, mtayarishaji wa rekodi, na mwigizaji.

8. Justin Bieber

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $747,000 sawa na TZS Bilioni 1.73 kwa Posti Moja.

Justin Drew Bieber ni mwimbaji wa Canada, mwigizaji na mtunzi. Alikuwa maarufu zaidi baada ya meneja wa vipaji kumgundua kupitia video zake za YouTube mwaka 2008.

7. Beyonce Knowles

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $770,000 sawa na TZS Bilioni 1.78 kwa Posti Moja.

Beyoncé Giselle Knowles-Carter ni mwimbaji wa Marekani, mwandishi, dancer, mwigizaji, na mfanyabiashara.

6. Selena Gomez

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $848,000 sawa na TZS Bilioni 1.96 kwa Posti Moja.

Selena Marie Gomez ni mwimbaji wa Marekani, mwigizaji, na mtayarishaji. Alikuwa maarufu zaidi baada ya kuonekana kwenye mfululizo wa vipindi vya televisheni vya watoto Barney & Friends.

5. Ariana Grande

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $853,000 sawa na TZS Bilioni 1.97 kwa Posti Moja.

Ariana Grande-Butera ni mwimbaji wa Amerika, mtunzi wa wimbo, na mwigizaji.

4. Kim Kardashian

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $858,000 sawa na TZS Bilioni 1.98 kwa Posti Moja.

Kimberly Kardashian West ni mwana televisheni wa Marekani, mrembo, socialite, mfanyabiashara, na mjasiriamali.

3. Cristiano Ronaldo

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $889,000 sawa na TZS Bilioni 2.0 kwa Posti Moja.

Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro GOIH ComM ni mchezaji wa soka wa Kireno ambaye anacheza kama mchezaji wa mbele wa klabu ya Italia Juventus na timu ya Taifa ya Ureno.

2. Kylie Jenner

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $989,000 sawa na TZS Bilioni 2.29 kwa Posti Moja.

Kylie Kristen Jenner mwana televisheni wa Marekani, mrembo, socialite, mfanyabiashara, na mjasiriamali.

1. Dwayne Johnson

Wanaolipwa Pesa Nyingi Kupost Tangazo Instagram (2020)

Analipwa Dollar $1,015,000 sawa na TZS Bilioni 2.35 kwa Posti Moja.

Dwayne Douglas Johnson, ambae pia anajulikana kwa jina lake la The Rock, ni mwigizaji wa Marekani, mtayarishaji, na wrestler mstaafu.

Mtandao wa instagram umebadilika sana toka ulipo anzishwa rasmi mwaka 2010, mwanzoni mtandao huu ulikuwa ni kwa ajili ya matumizi binafsi na kila mtu alikuwa akitumia mtandao huo bila kupata faida yoyote.

Miaka 10 baadae mtandao wa instagram umekuwa ni moja ya mitandao mihumu sana kwa sasa na watu wengi mbalimbali wamekuwa wakiendesha maisha yao kutokana na mtandao huo. Hivyo tumia vizuri akaunti yako ya instagram kwani inaweza kukubadilishia maisha siku moja.

Na hiyo ndio list ya watu 20 ambao wanapata mabilioni ya shilingi kuweza kupost tangazo kwenye mtandao wa instagram. Hivi kwa hapa Tanzania unadhani ni nani analipwa pesa nyingi kupost Tangazo kwenye akaunti yake ya instagram..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

1 comments
  1. Ahsanteni Tz tech kwa kutujuza hayo machache…fanyeni hivo piaa kwa kutuletea orodha ya juu ya watu maarufu wanaolipwa fedha nyingi apa kwetu ??

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use