Mtandao wa Kijamii wa TikTok Kusitishwa Hong Kong

Facebook, Google, Twitter, Zoom nazo kuacha kushirikiana na serikali ya Hong Kong
Mtandao wa Kijamii wa TikTok Kusitishwa Hong Kong Mtandao wa Kijamii wa TikTok Kusitishwa Hong Kong

Mtandao wa kijamii wa TikTok hivi karibuni umekubwa na matatizo mengi na kwa jinsi inavyo onekana mtandao huo unaendelea kukubwa na matatizo mengi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Reuters, hivi karibuni mtandao huo unategemewa kusitishwa huko Hong Kong huku ikiwa ni hatua ya kulinda data za watumiaji wake dhidi ya serikali ya mji huo.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, TikTok inategemea kusitisha kutoa huduma zake huko Hong Kong kutokana na kupitishwa kwa sheria mpya iliyoanza kufanya kazi hivi karibuni, sheria ambayo inazitaka kampuni zote zinazofanya kazi Hong Kong kutoa data za watumiaji wake kwa serikali ya mji huo.

Advertisement

Mtandao wa TikTok unamilikiwa na kampuni ya ByteDance ya nchini China, lakini kampuni hiyo inasema data ya watumiaji wake hazihifadhiwa nchini China – kitu ambacho kampuni hiyo iliiambia serikali ya India baada ya serikali ya India kupiga marufuku mtandao huo pamoja na programu zingine 58 kutoka nchini China.

TikTok imesema haijawahi kushiriki data zozote za watumiaji na serikali ya China hapo awali na haipo tayari kushiriki data za watumiaji wake na serikali yoyote. Lakini licha ya hayo, bado inaonekana kuwa programu hiyo inaweza kukutana na marufuku kutoka nchi zingine kwani hivi karibuni marekani nayo imeonekana kuwa iko mbioni kufungia programu hiyo.

Hata hivyo inasemekana kuwa sheria hiyo pia imezifanya kampuni nyingine kama Facebook, Google, Twitter, Zoom na nyingine, kuacha kushirikiana na serikali ya Mji huo kutokana na sheria hiyo mpya ambayo inazitaka kampuni zote kushiriki data za watumiaji wake na serikali ya mji huo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use