Jinsi ya Kuondoa Background Kwenye Video Yoyote

Huna haja ya kutumia programu yoyote wala kuwa na ujuzi wowote
Jinsi ya Kuondoa Background Kwenye Video Yoyote Jinsi ya Kuondoa Background Kwenye Video Yoyote

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Tanzania Tech basi ni lazima utakuwa unajua kuwa tulishawahi kuongelea njia za kuweza kuondoa background kwenye picha yoyote kwa urahisi na bila kutumia programu yoyote.

Kama bado hujui jinsi ya kuondoa background kwenye picha, basi nakushauri ukasome kwanza makala hiyo kisha unaweza kuendelea kusoma makala hii hapa. Kupitia makala hii nitaende kuonyesha njia mpya kabisa na rahisi ya kuweza kuondoa background kwenye video bila kutumia programu yoyote na bila kuwa na ujuzi wowote.

Njia hii ni bora na ni rahisi sana na unaweza kufanya hata kwenye smartphone yako, au kifaa chochote ambacho kina uwezo wa kutumia app za Android.

Advertisement

Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, video hiyo imefanikiwa kuondolewa background kwa asilimia 100 na mwisho umeona video hiyo ikiwa na weusi tu kwa nyuma huku kwa mbele mtu aliye onekana awali akiwa amebaki pale pale. Sasa najua unataka kujua jinsi ya kuondoa background kwenye video zako hivyo moja kwa moja twende nikueleze njia hii rahisi.

Kwa kuanza ingia kwenye tovuti hapo chini, kisha baada ya hapo bofya sehemu ya “Upload Clip” kama bado unayo video sasa endelea na chagua video yako kisha upload video hiyo kwenye website hiyo.

Tembelea Tovuti Hapa

Subiri baada ya muda kidogo na utaletewa video yako ikiwa imeondolewa background. Kumbuka usiondoke kwenye ukurasa huo subiri hadi video itakapo maliza.

Jinsi ya Kuondoa Background Kwenye Video Yoyote

Kwa sasa tovuti hii inasaidia kuondoa background kwenye video yoyote na unaweza kupata sehemu tu ya video hiyo na sio video yote. Pia kama unataka video yote unaweza kununua akaunti kwenye tovuti hiyo kwa kubofya sehemu ya Download High Resolution wakati wa kupakua video yako. Pia kumbuka unaweza kupakua video yako ikiwa kwenye mfumo wa GIF mfumo.

Na hiyo ndio njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuondoa background kwenye video ya aina yoyote. Kama unataka kujifunza zaidi basi hakikisha unatembelea channel yetu ya YouTube hapa kwani huwa tunajifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa vitendo.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use