Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuanzisha Tovuti ya Kisasa kwa Shilingi (Tsh) 3,000 Tu!

Kama umepata idea nzuri na unataka kufungua tovuti basi usijali soma hapa..
Tovuti Tovuti

Kuanzisha tovuti ni kitu ambacho watu wengi wanafanya sana siku hizi lakini watu wengi hutumia gharama kubwa sana kwenye kuanza kiasi kwamba idea au wazo linapo shindikana au kufa basi unajikuta umepata hasara kubwa sana, ndio mana leo Tanzania Tech tunakuletea makala hii ya kuanzisha tovuti ya kisasa kabisa kwa shilingi za kitanzania elfu tatu tu (3000)..!

Kwa kuanza bila kupoteza muda ni vyema kujua kuwa dollar inapanda na kushuka hivyo bei ya kuanza inategemeana na siku hiyo dollar iko vipi, makadirio niliyo yafanya ni kwamba haita zidi shilingi 3000 zaidi zaidi! inaweza kushuka na kuwa chini ya hapo yaani chini ya elfu tatu. Basi kwa kusema hayo moja kwa moja twende tuka angalie namna ya kupata tovuti ya kisasa kwa shiling elfu tatu 3000.

Advertisement

Mahitaji muhimu hapa ni kuhakikisha unaweza kununua kitu online yani kifupi unatakiwa uwe na Master Card au Visa Card ya benk yoyote iliyo sajiliwa na Internet Banking kama wewe ni mteja wa CRDB basi unaweza kubofya hapa kujua zaidi kuhusu kadi yako. Baada ya kusema hayo moja kwa moja twende tukaanze hatua hizi kwa umakini.

Hatua ya kwanza tumia link hii hapa kuingia kwenye akaunti ya Godaddy ili uweze kununua domain yako, unatumia link hiyo kwani kwa kutumia hiyo ndipo utaweza kupata ofa ya kuanza biashara yako mtandaoni kwa bei nafuu, baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa ambapo unatakiwa kuchagua jina la tovuti yako maarufu kama domain, hapa kuwa makini kwani pale unapo nunua domain yako ndio hiyo hiyo na utaweza kununua tena au kuanza biashara yako kwa shilingi 3000, kifupi ni kwamba ofa hii ni ya mara moja tu ukisha nunua ndio basi tena hutoweza kurudia tena.

Baada ya kununua domain yako nenda kwenye blogger na ujiunge na mtandao wa blogger, kama unataka kujua jinsi ya kujiunga na blogger bofya hapa endelea kwa kufuta maelezo yaliyoko kwenye video hiyo, ukimaliza kutengeneza blogger, ingia kwenye ukurasa wa blogger kisha bofya Settings alafu tafuta mahali palipo andikwa Publishing kisha bofya mahali palipo andikwa “setup 3rd party URL” anza kuweka jina la domain yako uku ukianza na www baada ya kumaliza bofya save kisha utaletewa maelezo yenye vitu ambavyo unatakiwa kuweka kwenye domain yako ambayo ulisajil hapo awali.

Baada ya kumaliza process zote hizo ingia kwenye akaunti yako ya Godaddy kisha bofya domain yako kisha kisehemu cha gear kisha chagua DNS Manage baada ya hapo nenda mpaka karibia na mwisho wa ukurasa utakuta sehemu imeandikwa ADD bofya hapo kisha chagua CNAME kwenye kichumba cha upande wa kushoto kisha kwenye Host weka www kisha kwenye Point to weka ghs.google.com alafu malizia kwa kubofya Save. Hatua inayofuata ni muhimu hapa unatakiwa kubofya ADD kisha weka CNAME kwenye chumba cha kushoto kisha kwenye host unatakiwa kuweka herufi zilizoko chini ya zile za www kisha kwenye point to weka zile zingine ambazo zina herufi nyingi, (kuelewa zaidi angalia video hapo juu).

Baada ya hapo bofya hapa ili kufungua ukurasa wa Google kisha sogea mpka kwenye hatua aliyo andikwa Step 2: Set up your domain with your blog bofya hapo ukurasa utafunguka zaidi kisha sogea mpaka hatua ya kumi kwenye namba hizi (kumbuka hii ni muhumu sana) .

  • 216.239.32.21
  • 216.239.34.21
  • 216.239.36.21
  • 216.239.38.21

Copy namba hizo moja moja na kisha nenda kaziweke kwenye domain yako kwenye akaunti ya godaddy, hizi ni muhumu kwani ndio zinafanya domain yako kufanya kazi vizuri usipo weka hizi domain yako itakuwa haifanyi kazi vizuri, (angalia video hapo juu ina maelezo na hatua kwa undani)

Ukimaliza kufuata maelezo yote haya kwa umakini utakuwa umefanikiwa kutengeneza tovuti yako ya kisasa kabisa kwa kutumia kiasi cha shilingi elfu tatu tu, kama unataka templents za bure kabisa za kuweka kwenye tovuti yako ili iwe ya kisasa zaidi bofya hapa kudownload. Kama una swali au kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza swali lako kupitia forum yetu hapa, pia kwa maoni unaweza kutumia fomu hiyo hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja ya teknolojia kwa njia ya video.

16 comments
  1. nimejalibu kununua hiyo domain kwa hela hiyo lkn imekataa wamenipa code lkn sijajua pa kuziweka ili ni nunue kwa bei ya $1 nifanyaje tafadhali

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use