Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuongeza Ulinzi wa Simu Yako na Aina Mpya ya Lock

Kama umesha zoea pattern, password na finger print basi hii hapa njia mpya
Ulinzi Ulinzi

Karibuni tena kwenye makala hii fupi, kwa kuanza najua wengi wetu tumesha zoea kuwa na ulinzi wa aina flani kwenye simu zetu, lakini kifupi ni kwamba inawezekana kwa sasa unaona ulinzi ulio nao kwenye simu yako hautoshi hivyo unataka kuongeza aina flani ya ulinzi ambayo ni ngumu mtu kuja au kugundua namna ya kufungua simu yako hivyo basi hii ikiwa ndio sababu leo Tanzania Tech tunakuletea aina hii mpya ya lock Screen ambayo na uhakika itakuwa ni ongezeko zuri na bora kwenye ulinzi wa simu yako.

Aina hii mpya ya ulinzi itakupa uwezo wa kulinda simu yako kwa kugusa kioo chako sehemu maalum ambazo wewe pekee ndio utakuwa unajua, hii ikiwa na maana hakuna mtu anaweza kujua ni wapi unagusa ili kufungua simu yako hivyo mtu hatoweza kufanya chochote kile kwenye simu yako, kingine ni kwamba lock hii itakupa uwezo wa kujua anae angalia simu yako kwani simu yako itapiga picha kwa yoyote anaetaka kutoa lock ya simu yako hivyo utakuwa unajua nani alietaka kufungua simu yako,

Advertisement

Vilevile utaweza kufunga simu yako kwa kugusa kioo cha simu yako mara mbili basi hakuna haja ya kubofya kitufe cha kuwasha simu, kifupi ni kwamba lock hii itaongeza ulinzi mara dufu zaidi ya ulinzi ulio uzoea kwa kawaida kwenye simu yako, basi moja kwa moja twende tukangalie njia hii.

Download App hii Hapa kisha endelea kwa kufuata hatua hizi kwenye video hapo chini, kuendelea kujifunza.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

6 comments
  1. Nimekwenda kwenye Google setting,security,Google play protect,scan device for security threats halo kuna tiki,sasa hii sehemu iliyoandikwa improve harmfulapp detection inamaana gani! naomba kufahamu kama nayo naweza kuweka tiki.

  2. Je ni kisha jisajili na hii huduma
    Simu yangu hata ikipotea naweza ipata kwa urahisi?
    ASANTE

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use