Jinsi ya Kufanya Simu Yako ya iPhone Kujaa Chaji kwa Haraka

Fanya simu yako ya iphone kujaa chaji kwa urahisi na haraka
kuchaji iPhone 1 kuchaji iPhone 1

Kuna wakati kuchaji simu yako ya iphone mpaka ijae kabisa inakuwa ni mthiani mkubwa sana na kwa bahati mbaya zaidi iphone nyingi hazina teknolojia ya fast charging hivyo kufanya simu yako kuchelewa sana kujaa chaji. lakini kwa kutumia njia hizi utaweza kufanya simu yako kujaa chaji kwa haraka zaidi kuliko inavyokua kawaida, Basi moja kwa moja twende tukangalie njia hizi.

  • Chaji kwa Kutumia Chaji ya iPad

Kama unayo iPad basi lazima pia utakuwa unayo chaji yake, kama unayo basi tumia chaji hiyo yenye wattage 10W au 12W kuchaji iphone yako hii itakusaidia kuliko kutumia chaji ya iPhone ambayo inatumia 5W.

  • Washa Flight Mode Unapokua Unachaji Simu

Mara nyingi simu yako ya iphone inatumia chaji kutokana na vitu mbalimbali ambavyo vinakua bado vinafanya kazi, lakini pale unapoweka Flight Mode umeme unaoingia kwenye simu yako unakuwa hautumiki kwa vyvovyote zaidi ya kuchaji battery ya simu yako, hivyo flight mode husaidia sana.

Advertisement

  • Zima Kabisa Simu Yako Unapochaji

Njia nyingine ni kuhakikisha unazima simu yako unapochaji, sababu zinafanana sana na hizo hapo juu kwani pale unapozima simu yako unaruhusu chaji kuingia kwenye battery pekee bila kutumika na kitu chochote ambacho kinafanya kazi pale simu yako inapokua imewashwa.

  • Chaji Simu Yako Kwenye Hali ya Hewa Iliyopowa

Hii ni muhimu sana kumbuka kuchaji simu yako kwenye hali ya hewa ambayo ina ubaridi kidogo, kwani kwa mujibu wa taarifa mbalimbali iphone ikichajiwa sehemu yenye joto kali basi uwezo wake wa kujaa chaji kwa haraka unakuwa ni mdogo sana, lakini pia kumbuka hali ya hewa kiwa baridi sana pia simu yako itakawai kujaa chaji hivyo hakikisha sehemu unayochaji simu yako iwe na hewa kidogo na sio yenye joto kupindukia au baridi kupindukia angalau (20 degrees celsius – 30 degrees celsius).

  • Zima Programu Zote Ambazo Hazina Umaana Muda Huo

Hatu ya mwisho kama unataka kuchaji simu yako ikiwa imewaka basi hakikisha unazima programu zote za iphone ambazo hazina umaana kwa muda huo au hutumii kwa wakati huo. Uzuri ni kwamba ili kufanikisha hili iphone imetengezewa sehemu maalum ya kufanya hivi sehemu hiyo inapatiaka kwenye Settings > Battery kisha washa sehemu iliyoandikwa Low Power Mode.

Basi kwa kufanya hivyo utakuwa umewezesha kufanya simu yako ya iphone kujaa chaji kwa haraka zaidi, kama utakuwa umekwama au unataka ushauri zaidi usisite kutuandikia kwenye maoni hapo chini pia kama unataka msaada zaidi unaweza kupata kupitia Forum yetu hapa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja yote ya teknolojia kwa njia ya video.

1 comments
  1. Asante Sasa tatizo jingine unakuta mtu charger ya simu Alo nunua nayo ilisha potea so atumie njia zip kupata charger nzur kwa simu yake?
    Naomba kusaidiwa

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use