Hatimaye Kampuni ya Airtel Tanzania Kuwezesha Mtandao wa 4G

Kwa sasa ni muhimu kufika kwenye maduka ya Airtel kwaajili ya kupata taarifa zaidi
Hatimaye Kampuni ya Airtel Tanzania Kuwezesha Mtandao wa 4G Hatimaye Kampuni ya Airtel Tanzania Kuwezesha Mtandao wa 4G

Baada ya kampuni za kutoa huduma za simu za Vodacom Tanzania na Tigo Tanzania kuwezesha mtandao wa 4G nchini Tanzania, hatimaye baada ya takribani miaka mitatu kampuni ya kutoa huduma za simu ya Airtel Tanzania nayo inategemea kuwezesha huduma hiyo ya 4G kwa wateja wake hivi karibuni.

Kwa mujibu ya maelezo ya mmoja wa watoa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania, huduma hiyo kwa sasa ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilika na watumiaji wa mtandao huo wa simu kwa sasa wanapaswa kubadilisha laini zao ili kuwezesha mtandao 4G kwenye laini zao ili mtandao huo utakapo wezeshwa waweze kupata huduma hiyo moja kwa moja.

Hatimaye Kampuni ya Airtel Tanzania Kuwezesha Mtandao wa 4G

Advertisement

Hata hivyo kwa sasa kama unayo laini ya simu ya Airtel Tanzania, unaweza kuangalia kama simu yako pamoja na laini kama zina uwezo wa 4G kwa kubofya *149*95#. Kama laini yako pamoja na simu vyote vinayo uwezo wa 4G basi endelea kusubiria pale utakapo pata ujumbe wa huduma hiyo kuanza kutumika. Kama laini yako haina huduma hizo basi unashauriwa kufika kwenye maduka ya airtel yaliyopo karibu na wewe ili kujua hatua za kufuata.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za uhakika kama huduma hiyo imesha anza kufanyakazi au inatarajiwa kuanza rasmi lini, kwa habari zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakupa ripoti kamili pindi tutakapo zipata. Kwa msaada zaidi kuhusu laini yako ya Airtel Tanzania hakikisha unatembelea maduka ya Airtel yaliyopo karibu na wewe au piga 100 kwaajili ya kupata msaada zaidi au tembelea tovuti ya Airtel Tanzania hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use