Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Mambo ya muhimu na jinsi ya kufungua blog kwa urahisi mwaha huu
Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Linapokuja swala zima la kufungua blog au kuanzisha blog ni vyema umekuja kwenye makala hii kwani kupitia hapa nitakujuza yote ya muhimu unayo takiwa kujua kabla na baada ya kufungua blog.

Kama wewe tayari ni mmoja wa watu wanao miliki blog au website basi ni muhimu sana pia kusoma makala hii kwani na uhakika utaweza kujifunza kitu. Basi bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Kufungua Blog

Advertisement

Blog ni Nini (Tofauti ya Blog na Website)

Kwa kuanza ni muhimu kujua kuwa napozungumzia blog hapa nina maana tovuti ya makala zinazo badilishwa kila siku, yani kama ilivyo Tanzania Tech au tovuti ya Millard Ayo, Bongo 5 na nyingine kama hizo.

Website ni tovuti ya biashara ambayo huwa na kurasa zisizo badilika, yaani kwa upande mwingine ni tovuti ya kutangaza biashara na mara nyingi huwa kwa lengo hilo tu, japokuwa inaweza kuwa na blog ndani yake.

Kama unataka kufungua tovuti ya kutangaza biashara basi basi endelea kutembelea Tanzania Tech tutakuletea makala hiyo. Kwa siku ya leo kama unataka kutengeneza blog ya maudhui, au makala basi endelea kusoma makala hii moja kwa moja.

Mambo ya Muhimu Kabla ya Kuanzisha Blog

Kwa kuanza ni vyema ufahamu kuwa kuna baadhi ya mambo ya muhimu ambayo unaweza kufuata kabla ya kuanza kutengeneza blog yako. Mambo hayo ni kama yafuatayo.

Lengo la Blog Yako

Ni muhimu sana kujua lengo la blog yako, hii itakusaidia sana kuchagua aina ya mifumo na mambo mengine ya muhimu ili kuweza kutengeneza blog yako kwa usahihi. Kwa mfano, kama lengo lako ni kujaribu kutengeza blog ya wazo fulani ambalo unalo, au hata kama wazo lako liko kwenye hatua za awali basi ni vyema kutumia mfumo kama Blogger.

Muhimu Kufahamu

Kifupi ni kuwa kama wazo lako liko kwenye hatua za awali ni vyema kutumia gharama ndogo iwezekanavyo kwenye uwekezaji wa kutengeneza blog yako, hii itakusaidia kuweza kujua uwezo wa wazo lako kabla ya kuamua kufanya uwekezaji zaidi.

Watumiaji wa Blog Yako

Katika ulimwengu huu wa mitandao ya kijamii ni vyema kujua kuwa watumiaji wako wanapatikana wapi, kama kwa asilimia kubwa unahisi watumiaji wako wanapatikana zaidi kwenye mitandao ya kijamii basi ni vyema kuanza na mitandao ya kijamii kama Instagram na Tiktok, kisha baadae kufungua blog kama kutakuwa na uhitaji huo.

Muhimu Kufahamu

Blog ni bora zaidi kama unataka kuwa na wasomaji wa uhakika, tofauti na mitandao ya kijamii mtumiaji hatoweza kuona makala zako za nyuma na pia utahitaji kupost kila siku ili kuweza kuendelea kupatikana na watumiaji wako.

Faida na Hasara za Blog Yako

Hakuna kitu chochote kisichokuwa na faida kikakosa hasara, ni vyema kuwaza hili kwani kuwa na blog ni kazi ya muda mrefu na kama wote tunavyojua muda siku zote unalipiwa. Yaani unapo poteza muda kufanya kitu fulani siku zote unatarajia matokeo fulani hii ni sawa pia pale unapotaka kuanzisha blog.

Muhimu Kufahamu

Kama unatarajia kuanzisha blog kwa ajili ya kutoa elimu ya bure basi ni vyema ujue kuwa unahitaji muda wa ziada kutoa elimu hiyo na hivyo inamaanisha kugawa muda wako kwenye jambo hilo bila kupata faida yoyote.

Lakini pia upande wa pili wa faida, unaweza kupata faida kwa kuweka matangazo kwenye blog yako na kulipwa pesa, au kufanya makala zako za kulipia hapo baadae utakapo pata wasomaji zaidi. Ni vizuri kujua haya ili kujua jinsi utakavyo jipanga kuanzisha blog yako kulingana na muda wako.

Njia za Kuingiza Pesa Kupitia Blog Yako

Kwa kumalizia kwenye hatua za muhimu kabla ya kuanzisha blog, ni vyema ufahamu kuwa ni muhimu sana kufikiria njia za kutengeneza pesa kupitia blog yako. Hii itakusaidia sana kujua jinsi ya kuandika makala zako kwa ajili ya kutengeneza pesa hata hapo baadae.

Muhimu Kufahamu

Kuwaza njia za kutengeneza pesa kupitia blog yako mapema kunaweza kukusadia kujua jinsi ya kuanza blog yako, kwani unaweza kutengeneza makala zinazoendana na mfumo wa kutengeneza pesa hapo baadae, yaani kama unarajia kutengeneza pesa kwa mfumo wa Adsense basi ni muhimu sana kuanza blog yako kwa lugha ya Kingereza.

Lakini pia kama unataraji kupata udhamini kupitia makampuni ya ndani basi unaweza kuandika makala zinazoendana zaidi na bidhaa au huduma zinazotolewa na makampuni husika ili kuvutia wadhamini zaidi. Hii ina maana kuwa tengeneza makala ambazo wadhamini wataweza kuweka matangazo kwenye blog yako bila wao kuharibu mtazamo wa kampuni yako.

Hatua za Jinsi ya Kufungua Blog

Baada ya kuangalia mambo ya muhimu moja kwa moja twende kwenye hatua za jinsi ya kufungua blog. Unaweza kufungua blog kwa kutumia simu au kompyuta yako, kitu cha muhimu ni kuwa na Internet kwenye kifaa husika. Kupitia hatua hizi za awali nitakuonyesha jinsi ya kufungua blog kupitia mtandao wa blogger na wordpress.

Jinsi ya Kufunga Blog Kupitia Blogger

Kwa kutumia simu yako au kompyuta, moja kwa moja tembelea tovuti ya blogger kwa kubofya link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya kutembelea tovuti hii hakikisha umeingia kwenye akaunti yako ya Google au Gmail kama huna akaunti hakikisha una tengeneza akaunti. Baada ya hapo bofya sehemu ya Create Your Blog.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Baada ya hapo changua jina unalotaka linonekane kwenye blog yako unaweza kuchagua jina kwa kuliandika moja kwa moja kwenye sehemu ya Display Name.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Baada ya hapo moja kwa moja bofya Next kisha utapelekwa kwenye ukurasa wa kuchagua link ya blog yako hakikisha unachagua link ambayo ni inapatikana na utajua hilo kwa kuona maandishi yaliyo andikwa This blog address is Available.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Bofya Next kuendelea kwenye hatua inayofuata ambao utatakiwa kuandika tena jina la blog yako na kisha malizia kwa kubofya Finish.

Baada ya hapo utapelekwa kwenye kurasa ya blogger na unaweza kuendelea kupost kwa kubofya kutufe cha new post na kuanza kupost.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Kwa kufanya hatua hizo utaweza kutengeneza blog yako kupitia mtandao wa blogger. Moja kwa moja utaweza kuendelea kuandika makala zako na kupost moja kwa moja.

Jinsi ya Kufungua Blog Kupitia WordPress

Kwenye hatua zinazofuata twende tukangalie jinsi ya kufungua blog kupitia mtandao wa WordPress, njia hii ni rahisi na pia ni bure kama ilivyo mtandao wa blogger. Kwa kuanza tembelea tovuti ya wordpress kwa kubofya sehemu link hapo chini.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa maalum, bofya sehemu Get Started kuanza kutengeneza blog yako.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Baada ya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye sehemu ya kutengeneza akaunti, unaweza kutumia akaunti yako ya Google kutengeneza akaunti ya WordPress kwa kubofya Continue with Google.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Baada ya hapo utaweza kutengeneza akaunti yako na utapelekwa kwenye ukurasa maalum wa kuchagua link ya blog yako.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Andika jina la link yako bila kuacha nafasi kisha maliza kwa kuchagua link ya bure ambayo itakuwa na wordpress.com, pia imeandikwa Free.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Chagua kwa kubofay seleke kisha utaona sehemu ya Your Domain, bofya Continue kuendelea ili kuhifadhi link yako.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa wa kuchagua vifurushi hakikisha unachagua, Free kifurushi cha kwanza upande wa kulia.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Kwenye ukurasa unaofuata chagua sehemu ya kwanza ambayo ni Write and Publish, kisha malizia kwa kubofya Continue.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Baada ya hapo utapelekwa kwenye ukurasa wa kuandika jina la blog yako, hili ni jina hivyo kama lina neno zaidi ya moja unaweza kutengenesha. Baada ya hapo malizia kwa kubofya Continue.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Kwenye ukurasa unafuata bofya Skip to Dashboard inayopatikana juu upande wa kulia, moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa blog yako tayari kwa kuanza kuandika makala zako. Bofya sehemu ya Post, kisha chagua new Post kuanza kupost.

Jinsi ya Kufungua Blog Kuanzia Mwaka 2024 na Kuendelea

Hitimisho

Kwa kufuata hatua zote hapo juu utaweza kujifunza kutengeneza blog yako kwa urahisi na haraka, kumbuka njia hizi unaweza kufanya kwenye kompyuta au hata kwenye smartphone yako. Kama unataka kujua zaidi kuhusu blog na jinsi ya kuendesha blog hakikisha unaendelea kutembele Tanzania Tech kila siku, pia pakua app ya Tanzania Tech kupata habari za teknojia kwa urahisi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use