Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone

Utaweza kuedit na Kusign Document yoyote ya PDF kupitia simu yako
Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone

Kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi basi ni wazi kuwa umeshawahi kukutana na PDF, PDF maana yake ni “Portable Document Format” hii ikiwa ina maana ni aina ya document ambayo ni nyepesi zaidi au rahisi.

PDF ni rahisi kutumika kwa mtu yoyote yule kwani hata sasa unaweza kutuma aina hiyo ya document kupitia WhatsApp, mbali ya hayo kama unataka ku-print document yoyote kwa haraka basi ni vyema kuweka kwenye PDF kwani format hii hurahisisha mambo mengi.

Pamoja na faida nyingi za PDF, ni wazi kuwa linapokuja swala zima la kuedit PDF ni wazi kuwa imekuwa ni kazi ngumu sana. Tofauti na document kama DOCX ambayo huweza kufunguka na kuedit kwa urahisi, PDF ni ngumu sana kuedit mpaka hapo utakapo badilisha format.

Advertisement

Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi sana ambayo unaweza kutumia kuweza kuedit PDF kupitia simu yako ya mkononi ya Android. Njia hizi zinafanya kazi kwa urahisi ikiwa pamoja na mambo mengine zaidi ambayo yanaweza kurahisha maisha yako ya kila siku.

Kwa kuanza unacho takiwa kufanya ni kudownload app hapo chini kisha install kwenye simu yako, app hii imekuwa activated hivyo unaweza kutumia bila matangazo na bila kulipia.

Download App Hapa

Jinsi ya Ku-sign na Ku-edit PDF Kupitia Smartphone

Kama unavyoweza kuona kupitia picha hapo juu, utaweza kuedt PDF kwa kuchagua sehemu ya PDF, na pia utaweza kusign PDF kwa kutumia sehemu hapo juu, pamoja na mambo mengine mengi kama vile kubadilisha Office kuwa PDF yaani “DOCX kuwa PDF” au “PDF kuwa DOCX”.

Pia utaweza kuunganisha page tofauti za PDF kwa kutumia sehemu ya Merge PDF, na utaweza kupata document moja ikiwa na page mbalimbali. Bila kusahau sehemu ya kuscan picha yoyote kuwa PDF, kama ilivyo programu ya Cam Scanner.

Bila shaka programu hii inaweza kukusaidia wewe kufanya mambo mbalimbali hasa kama wewe ni mwanafunzi wa chuo, mfanyakazi au hata mtu yoyote anajihusisha na maswala ya office.

Kama unataka kujifunza zaidi, unaweza kusoma hapa jinsi ya kutengeneza business card kwa urahisi kwa kutumia smartphone yako. Pia kama unataka kujua jinsi ya ku-edit PDF kwa kutumia kompyuta basi unaweza kusoma makala yetu hapa. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea Tanzania tech.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use