in

Tengeneza Pesa Kupitia Adsense kwenye Blog ya Kiswahili

Njia mpya, rahisi na halali kwa asilimia 100 ya kupata matangazo ya Adsense

Tengeneza Pesa Kupitia Adsense kwenye Blog ya Kiswahili

Adsense ni moja kati ya mtandao ambao huwalipa zaidi blogger na waandishi mbalimbali, lakini kwa sasa mtandao huu bado haufanyi kazi kwa blogs za lugha ya Kiswahili na hii imekuwa ni tatizo kwa waanzilishi mbalimbali kutokana na kukosa mapato ya mtandao huo ambao ndio unao ongoza kwa kulipa waandishi mbalimbali wa blogs duniani.

Kuliona hili leo Tanzania tech tumekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kutengeneza pesa kwa kutumia mtandao wa Adsense kupitia blog au website yoyote ya Kiswahili. Njia hii inafanya kazi kwa asilimia 100 na unaweza kuanza kuifanya kupitia blog au website yako ya Kiswahili bila gharama za aina yoyote.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Mahitaji Muhimu

Kitu cha muhimu ni kuhakikisha tayari unayo website au blog ambayo inafanyakazi kwa asilimia 100, pia ni muhimu kuwa na akaunti ya Google kwani tutaenda kutumia blogger kuweza kuweka matangazo kwenye tovuti yako ya Kiswahili, hivyo hakikisha unayo blogger kama huna unaweza kujifunza jinsi ya kutengeneza blogger kupitia hapa.

Hatua za Muhimu

Baada ya hapo sasa unaweza kuendelea kwenye hatua zinafuata, Unatakiwa kufuata hatua zote kupitia video hapo chini. Ni muhimu sana kufuata hatua zote kabla ya kuendelea kwenye hatua zinazofuata baada ya video hapo chini.

Download Hapa Link Pesa

Baada ya kudownload, kuinstall pamoja na kuweka kutengeneza mfumo huu, sasa hatua zinazofuata ni kuweka custom domain kwenye blogger yako, unaweza kutumia domain au subdomain ya website au blog ambayo tayari unayo. Google hupokea maombi ya matangazo kutoka kwenye domain na subdomain hivyo usiwe na wasiwasi na hilo.

Kama ufahamu jinsi ya kuweka custom domain unaweza kufuata maelekezo hapa au pia unaweza kuendelea kutumia subdomain ya .blogspot.com, lakini ni muhimu kutumia custom domain kama unataka kuwa approve au kupewa haraka matangazo kupitia mtandao wa Goolgle Adsense.

Baada ya hapo natumaini utakuwa umeweza kuweka matangazo kwenye blog yako ya kiswahili, njia hii itakusaidia sana kama unayo website yenye link nyingi ambazo zinatoka nje ya blog yako kwa mfano kama unayo website ya kudownload au website yoyote yenye external link.

Kama kuna mahali umekwama kwa namna yoyote unaweza kuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini, pia kama unataka kuona mfano wa blog ambayo nimeweka matangazo ya aina hii basi unaweza kutembelea tovuti hapo chini.

Angalia Mfano Hapa

Ndani ya tovuti hiyo ya mfano bofya link yoyote ambayo inatoka nje ya tovuti hiyo yani link yoyote ambayo sio teknolojia.tk na ambayo sio link ya social media. Post yoyote itakayo ongezwa yenye link ambayo inatoka nje ya tovuti hiyo itakuwa na matangazo automatically bila mimi kufanya kitu kingine chochote.

Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia hakikisha unajiunga na channel yetu ya Tanzania tech kupitia mtandao wa YouTube hapa kwa ajili ya kupata maujanja kama haya kwa wakati.

Tengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Simu Yako (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments