in

Apps Nzuri za Kuangalia Mpira Kupitia Simu ya Android

Angalia filamu, mpira wa miguu pamoja na channel mbalimbali kupitia app hizi

Apps Nzuri za Kuangalia Mpira Kupitia Simu ya Android

Siku hizi teknolojia imekuwa inaleta urahisi sana wa kupata unacho kitaka kwa haraka zaidi, kuliona hili leo nimekuandalia list ya app nzuri za Android ambazo zinaweza kusaidia kuweza kuangalia TV na mpira Live kwa haraka zaidi kupitia simu yako ya mkononi ya Android.

App hizi zimeondoloewa matangazo hivyo hazipatikani kwenye soko la Play Store, pia kama unataka kudownload app hizi zenye matangazo unaweza kutafuta jina husika kupitia soko la Play Store. Basi baada ya kusema hayo twende tukangalie apps hizi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

App Bora

App hii iliyotajwa kwenye video hapo juu ni moja kati ya app bora sana ya kufuatilia michezo yote duniani, kupitia app hii utaweza kufanya mambo mengine sana ikiwa pamoja na kuangalia michezo yote live ikiwa pamoja na kufuatilia matokeo mubashara kabisa. Kama unataka kufuatilia mpira live basi hii ndio app bora ya kuwa nayo.

Download App Hapa

JioTV

JioTV

JioTV ni moja kati ya app maarufu sana kwa kuonyesha Mpira Live pamoja na movie mbalimbali, App hii inakupa channel nyingi ambazo huwezi kuzipata mpaka ulipie, hivyo basi kama wewe ni mpenzi wa michezo mbalimbali pamoja na filamu basi nakusihi download app hii kisha utaniambia kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Download App Hapa

BeeTV

beetv

Kama wewe ni mpenzi wa filamu pamoja na tamthilia mbalimbali basi ni vyema kujaribu app hii ya BeeTV kwenye simu yako ya Android. App hii itakupa filamu mpya kwa urahisi pamoja na tamthilia mpya moja kwa moja kupitia simu yako, kama kuna filamu fulani ulikuwa unaitafuta na huipati basi jaribu kuitafuta kupitia app hii ya BeeTV.

Download App Hapa

Live TV

live-tv

Live TV ni app nyingine nzuri sana ambayo inaweza kukusaidia kuweza kuangalia michezo mbalimbali kupitia simu yako ya mkononi ya Android. App hii ni nzuri kwa sababu inakupa urahisi wa kutumia hasa kama utaki kupoteza muda mwingi kutafuta unacho kitaka, unaweza kudownload app hii kupitia link hiko hapo chini.

Download App Hapa

WhiteIPTV

WHITEIPTV

WhiteIPTV ni moja kati ya app zenye TV nyingi kuliko app zote kwenye list hii, App hii inakupa uwezo wa kuangalia channel karibia zote zilizopo kwenye king’amuzi cha DSTV, pia app hii ni rahis sana kutumia na inafanya kazi kwa haraka. Unaweza kudownload app hii kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

GaTo TV

gatotv

Gato TV ni app nyingine nzuri kuangalia michezo mbalimbali, app hii ina mkusanyiko wa channel mbalimbali za michezo ambazo ulikuwa huwezi kuzipata kwenye app nyingine. App hii nayo pia ni rahisi sana kutumia na unaweza kuipata kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Na hizo ndio app ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo kama unataka kujua app nyingine nzuri za kujaribu kwenye simu yako unaweza kusoma hapa makala yetu ya app nzuri iliyopita. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Amani Joseph

Apps Nzuri za Kuangalia Mpira Kupitia Simu ya Android

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps za Muhimu Kuwa Nazo Kwenye Simu Yako (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments