in

Apps #25 Apps Nzuri za Kusaidia Simu Kudumu na Chaji

Jaribu apps hizi kuweza kusaidia simu yako kudumu na chaji kwa muda mrefu

Apps za kusaidia simu kudumu na chaji

Simu kutokudumu na Chaji ni tatizo la simu nyingi sana za Android siku hizi, lakini pamoja na tatizo hili kuongezeka kila siku ni kweli kuwa matumizi ya simu nayo pia yamekuwa makubwa sana na pengine hii ndio sababu ya simu nyingi kutokuwa na uwezo wa kudumu na chaji kwa muda mrefu.

Lakini kama kwa namna yoyote umekuwa ukiona matumizi yako ni ya kawaida na bado simu yako ya Android inaisha chaji kwa haraka sana basi ni wakati wa kujaribu njia nyingine kama hizi za Apps nzuri za kukusaidia kufanya simu yako idumu na chaji kwa muda mrefu.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Njia ya kutumia apps hizi ni nzuri kwani inakusaidia kuweza kusitisha baadhi ya kazi ambazo zinafanywa na simu yako ambazo zinakuwa hazina ulazima kwa namna moja ama nyingine. Basi bila kupoteza muda let’s get to it.

AccuBattery

Accu​Battery
Price: Free

AccuBattery ni moja kati ya App nzuri sana, App hii inauwezo wa kukusaidia kufanya simu yako idumu na chaji kwa muda mrefu, app hii pia inauwezo wa kukuonyesha mambo mbalimbali kama vile muda gani battery yako inatumia kujaa au kuisha pale unapoichaji, pia ina kuonyesha kiasi cha chaji kinacho tumiwa na kila app kwenye simu yako.

Amplify

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye simu ambazo ziko rooted basi na hakika utapenda app hii ya Amplify. App hii inauwezo wa kuangalia mfumo mzima wa android na kuonyesha app zinazotumia chaji sana na ikiwa pamoja na njia za kuweza kuzima apps hizo. Kama unasimu ambayo iko rooted basi jaribu app.

Greenify

Greenify
Price: Free

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya tanzania tech nadhani utakuwa umesha sikia tukitaja app hii mara nyingi sana. App hii ni nzuri sana ya kuweza kufanya simu yako idumu na chaji. App hii inauwezo mzuri wa kuzima apps ambazo zinatumia chaji nyingi na kufanya simu yako kudumu na chaji zaidi.

Avast Battery Saver

Avast Battery Saver
Price: Free+

Avast battery saver ni app nyingine nzuri sana ya kufanya simu yako kudumu na chaji, App hii inauwezo wa kuonyesha kiasi cha chaji kinacho tumiwa na apps mbalimbali kwenye simu yako, vilevile app hii inakupa uwezo wa kuzima apps hizo kwa kubofya kitufe kimoja tu.. Kama unatafuta app nzuri na rahisi kutumia basi unaweza kutumia app hii.

Gsam

GSam Battery Monitor

Gsam ni app nzuri kwa wale wanapenda kujua zaidi kuhusu tabia za apps mbalimbali kwenye simu zao. App hii inakupa uwezo wa kujua kuhusu app zinazo tumia chaji kwa wingi ikiwa pamoja na settings mbalimbali ambazo labda umeseti kwenye simu yako ambazo zinatumia chaji kwa wingi.

Kaspersky Battery Saver

App nyingine nzuri ambayo itakusaidia kufanya simu yako idumu na chaji ni app ya kaspersky battery saver. App hii ni nzuri na kweli inauwezo mkubwa wa kufanya simu yako iweze kudumu na chaji kwa muda mrefu.

Na hizo ndio apps nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kama unataka kujua apps nyingine nzuri za kuongeza ulinzi kwenye simu yako ya Android basi soma makala hii hapa. Kwa habari zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Apps #25 Apps Nzuri za Kusaidia Simu Kudumu na Chaji
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2024)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments