in

Jinsi ya Kuweka Muonekano wa Giza Kwenye Instagram (Android)

Muonekano huu utakusaidia hasa wakati wa usiku kuzuia mwanga mbaya machoni

Jinsi ya Kuweka Muonekano wa Giza Kwenye Instagram (Android)4:01

Kama wewe ni mmoja wa watumiaji wa programu mbalimbali basi ni wazi kuwa unajua siku hizi programu nyingi zinakuja na muonekano wa Giza au Dark Mode. Kwa bahati mbaya sio kila simu inakuja na uwezo wa kuweka Dark Mode au muonekano wa giza kwenye apps mbalimbali.

Lakini kutokana na kuwa muonekano huu ni muhimu hasa wakati wa usiku, leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuwasha muonekano huu wa giza au dark mode kwenye mtandao wa Instagram kupitia simu yoyote ya Android. Njia hii ni rahisi na fupi hivyo sitochukua muda wako mwingi zaidi nikusihi tu uniazime dakika zako nne tu ili tujifunze maujanja haya kwa pamoja.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Baada ya kuangalia video hiyo, unaweza kupata app iliyotajwa kwenye video hapo juu kwa kupakua kupitia soko la Play Store kupitia link hapo chini.

Dark Mode
Price: Free

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza, kujifunza jinsi ya kuwasha muonekano huo wa Giza kwenye kompyuta yako ya Windows au MacOS. Njia zote ni rahisi sana na unaweza kufanya kwa haraka bila kupoteza muda. Kwa maujanja zaidi hakikisha una Subscribe kwenye Channel ya Tanzania Tech hapa.

Jinsi ya Kutumia Aina Mbalimbali za AI Kwa Wakati Moja

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments