in

Tofauti Kati ya Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart

Fahamu hapa tofauti kati ya simu hizi mbili kutoka Vodacom na Tigo

Tofauti Kati ya Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart

Kama upo nchini Tanzania basi najua utakuwa unajua kuhusu Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart, simu hizi zimekuwa zikitangazwa sana hapa Tanzania kutokana ubora wake ikiwa pamoja na uwezo wake wa 4G.

Sasa kutokana na kuwa simu hizi zinatoka mitandao tofauti, leo nimeona nikuletee makala yenye uchambuzi kidogo kuhusu simu hizi mbili ikiwa pamoja na tofauti kati ya simu hizi mbili ambazo zimekuwa gumzo sana kwa sasa hapa Tanzania kupitia mitandao hii ya Vodacom na Tigo Tanzania.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Uwezo wa 4G

Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart ni simu ambazo zinasifika sana kwa kuwa na uwezo wa 4G, lakini kama hujui uwezo wa simu hizi kuwa na 4G ni kutokana na mfumo mpya wa simu za namna hii ambazo zinatumia mfumo mpya wa KaiOS. Mbali ya mfumo huo ambao ndio unawezesha mambo yote, simu hizi pia zinakuja na chip ambazo ndio zinawezesha simu hizi kuwa na uwezo wa 4G LTE.

Tofauti Kati ya Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart

Simu zote za Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart zinakuja na uwezo sawa wa 4G LTE zikiwa na uwezo wa LTE1 Cat-1, 10 Mbps DL / 5 Mbps UL.

Sifa na Muundo

Kwa upande wa sifa simu hizi mbili zinakuja na sifa zinazofanana kabisa lakini zinatofautiana kidogo, Tigo Kitochi 4G Smart inakuja na battery kubwa kidogo kuliko Vodacom Smart Kitochi, hii inasababisha simu hizi kuwa na uwezo wa tofauti wa kudumu na chaji huku Tigo Kitochi ikiwa na uwezo wa battery yenye uwezo wa hadi 1,900 mAh Battery yenye uwezo wa kudumu na chaji hadi masaa 28 ukiwa unaongea, hayo sio maneno yangu bali ni maneno yaliyo andikwa kwenye tovuti ya kampuni ya Energizer.

Tofauti Kati ya Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart

Kama ulikuwa hujui Tigo Kitochi 4G Smart ni sawa kabisa na simu kutoka Energizer inayoitwa ENERGY E241S ambayo nayo inakuja na muundo na sifa zinazo fanana kabisa na sifa za simu hii mpya ya Tigo Kitochi 4G Smart. Unaweza kusoma sifa kamili za Tigo Kitochi 4G Smart hapo chini.

Pia sifa hizo zinafanana kabisa na sifa za Vodacom Smart Kitochi isipokuwa battery ambapo Vodacom smart kitochi ambayo kwa mujibu wa tovuti ya KaiOS, simu hii inakuja na battery yenye uwezo wa 1,450 mAh Battery.

 

Sasa basi kwa kuhitimisha ni vyema ujue kuwa simu hizi zote mbili zinafanana sana kwa sifa lakini zinatofautiana kwa muonekano, bei pamoja na uwezo wake wa battery. Kwa kusoma hayo basi natumaini utakuwa umepata angalau idea ya ni simu gani ambayo itakufaa zaidi. Kama unataka kuona tofauti ya simu hizi zikiwa kwa pamoja unaweza kusoma zaidi hapa.

Tofauti Kati ya Vodacom Smart Kitochi na Tigo Kitochi 4G Smart

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, pia kama una swali au maoni au ushauri unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Vodacom Smart Kitochi vs Tigo Kitochi 4G Smart

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

36 Comments

  1. Aisee kaka shukrani sana kwa maelezo yako yameweza kunisaidia kuweza kufanya maamuzi sahihi kitochi gani cha kununu. Asante sana.
    Lakini nina swali moja tuu hapa, nimeona hii ya vodacom ni 3G, ni kweli 3G au ni 4G kama ya Tigo?