Yakujua Kabla ya Kununua Simu Mpya ya Samsung Galaxy Note 7

Mapitio ya simu mpya iliyozinduliwa hivi karibuni ya samsung note 7
Samsung Galaxy Note 7 Samsung Galaxy Note 7

Kwa namna yoyote ile Samsung Note 7 ni simu bora sana ukilinganisha na simu nyingine ambazo samsung imeshatoa mwaka huu, utengenezaji wa kioo chenye muonekano bora pamoja na battery yenye kudumu pia na resolution bora sana inawezekana kabisa samsung note 7 ikiwa ndio simu bora sana ndani ya mwaka huu. Nitaendelea kukwambia kuwa samsung note 7 ni moja kati ya simu za Android zenye nguvu kubwa pamoja na uwezo mkubwa sana kitu ambacho Samsung wanaonekana kukizingatia sana mwaka huu.

Lakini tusishie hapo tu.. kama unataka kununua samsung note 7 inawezakana kabisa ni kutokana na sifa fulani inayopatikana kwenye simu hiyo, mimi binafsi ningependa kuwepo nayo sababu ya (Iris Scanner) hii ni moja kati ya sifa mpya kabisa za mwaka huu ambazo samsung wamekuja nazo kwa watumiaji wake wapya wa Note 7, lakini tusiende haraka sanaa kutokana na maoni ya blog nyingi za habari za teknolojia ambazo wamepata nafasi ya kuwa na simu hii kwa ukaribu ina wezekana ukawa (disappointed) kidogo kwani wengi wanasema kuwa ni vizuri usitegeme sifa hiyo kutokana na kuwa inasemekana haifanyi kazi kwa haraka ukilinganisha na ile ya (Fingerprint) inayopatikana kwenye Simu hiyo pamoja na Samsung galaxy S6 na S7.

Pamoja na kwamba Iris Scanner inawezakana kuwa ni tatizo kidogo kwa sasa lakini hairudishi chini simu hii kwani uwezo wake pamoja na sifa zingine za simu hii kama vile kamera yenye muonekano bora pamoja na IP68 waterproof ni sifa zenye kufanya simu hii kuendelea kuwa bora na ya kisasa ndani ya mwaka 2016 na pengine mpaka mwaka 2017.

Advertisement

Pia hatuwezi kusahau SPen kwani hii ni moja kati ya sifa zinazoifanya Samsung Note zote kuwa tofauti na simu nyingine, mwaka huu samsung wameongeza kuwa japokua SPen inaacha nafasi kwenye simu yako usidhani kuwa simu yako iko hatarini hapana kwani samsung wameweka wazi kuwa simu hii ni (water resistant) na inauwezo mkubwa wa kuzuia kiwango maalumu cha maji yasidhuru simu yako. Sifa nyingine za simu hii ya kisasa kutoka Samsung ni kama zifuatazo:

SIFA ZA SAMSUNG NOTE 7

 • 5.7-inch, quad-HD Super AMOLED display
 • Octa-core CPU
 • 4GB RAM
 • 64GB internal storage
 • microSD expansion
 • S-Pen
 • Android 6.0.1
 • Fingerprint and Iris scanner
 • USB-C
 • Fast and wireless charging
 • 3,500 mAh battery
 • IP68 water resistance
 • 153.5 x 73.9 x 7.9mm, 169g
 • 12MP camera, f1.7 aperture
 • 5MP selfie camera
 • Manufacturer: Samsung
 • Review Price: TZS 2105983.09

Kwa kupata habari zaidi unaweza kuungana nasi kupitia barua pepe (email) na tutakujulisha pindi tu habari mpya itakapo ingia kwenye tovuti yetu ya Tanzania tech, pia unaweza kutufuata kwenye mitandao ya kijamii ya  facebook, Instagram, Twitter na Youtube Channel ili kupata video za habari na mafunzo ya teknolojia mbalimbali.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use