Yakujua Kabla ya Kununua Simu Mpya ya iPhone 7

Haya ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kuyajua kabla ya kununua simu Mpya ya iPhone 7 au iPhone 7 plus
iphone 7 iphone 7

Kama unataka kununua simu mpya ya iPhone 7 au 7 plus yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo ni muhimu sana kuyajua kabla ya kununua simu hiyo, kama tunavyojua simu hiyo mpya siku ya tarehe 16 september 2016 ndio inaanza kusambazwa kote duniani hivyo ni muhimu sana kujua haya kabla simu hiyo haijafika ulipo.

Apple kupitia simu yake ya iPhone 7 mwaka huu imekuja na mtazamo tofauti kwa wateja wake kwani imeamua kujikita sana kwenye teknolojia mpya zaidi kuliko kukidhi haja ya wateja wa zamani, hivyo kama unataka kununua iPhone 7 ukitegemea kukutana na mambo uliyoyazoea hapo awali basi iPhone 7 itakua sio kwaajili yako lakini kama unatafuta Simu ya kisasa yenye teknolojia mpya pamoja na sifa mbalimbali za kioo na kamera angavu basi iphone 7 na 7 plus ni simu bora kwaajili yako.

Advertisement

Zaidi kama wewe ni mpenzi wa kamera mwaka huu iPhone imekuja na iPhone 7 plus ambayo sasa inayo kamera mbili zenye uwezo wa 12MP kila moja hivyo kama wewe unaitaka simu hii mpya kwaajili ya kamera basi hii ni simu bora sana ya kununua kwa-ajili yako. Pia simu hii mpya imekuja na nafasi zaidi ikiwa imeachana na ukubwa wa GB 16 na Pia GB 64 hivyo kama bado unatafuta simu hizi zenye GB 16 na GB 64 basi ni vyema ukajua mapema kwamba simu hizi hazipo tena kwenye toleo hili jipya.

Lakini kizuri zaidi ni kwamba iPhone sasa imekuja na nafasi zaidi na-maana kwamba simu hizi sasa zina anzia GB 32, GB 128 na GB 256 hivyo hii ni habari njema kwa watumiaji wa simu hizi za iPhone 7 kwani simu yenye memory ya chini itanzia GB 32 na kuendelea.

Pia kinginge kizuri simu hii inakuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa iOS 10 ambapo ni mfumo unaokuja na sifa mpya mbalimbali ikiwemo Music Player mpya, App Store pamoja na mambo mengine mbalimbali pia kama ulikua unataka kujua sifa za simu hii kwa ujumla sifa hizo ni kama zifuatazo.

SIFA ZA iPHONE 7

 • 4.7 inches, LED-backlit IPS LCD display
 • Apple A10 Fusion Quad-core CPU
 • 2GB RAM
 • 32/128/256GB internal storage
 • microSD expansion Haipo
 • iOS 10
 • Fingerprint
 • USB v2.0, reversible connector
 • Fast and wireless charging
 • Non-removable Li-Ion battery
 • IP68 water resistance
 • 138.3 x 67.1 x 7.1 mm (5.44 x 2.64 x 0.28 in)
 • 12 MP, f/1.8, phase detection autofocus, OIS, quad-LED (dual tone) flash
 • 7 MP, f/2.2, 1080p@30fps, 720p@240fps, face detection, HDR, panorama selfie camera
 • Manufacturer: Apple
 • Bei kwa GB 32  TZS 1419882.20
 • Bei kwa GB 128 – TZS 1638662.20
 • Bei kwa GB 256 – TZS 1857442.20

Bei zote ni kwa viwango vya kubadilisha fedha vya tarehe 10 September 2016 hivyo bei inaweza kupanda au kushuka kutokana na kupanda au kushuka kwa dollar.

Ili kuendelea kujua kuhusu simu hii mpya ya iPhone 7 unaweza kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use