in

Kampuni ya Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto One Micro

Simu mpya ya bei nafuu kutoka kampuni ya motorola

Kampuni ya Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto One Micro

Motorola One Macro ni simu mpya kutoka kampuni ya Motorola. Simu hii inakuja na kioo cha inch 6.2 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya IPS LCD, kioo hicho inakuja na uwezo wa kuonyesha picha zenye resolution ya hadi pixel 720 x 1520.

Motorola One Macro inakuja na kamera tatu kwa nyuma, kamera kuu ya megapixel 12- kamera ya pili yenye megapixel 2, na kamera nyingine yenye megapixel 2, kamera zote zinachukua video za hadi pixel 1080p@30/60/120fps. Kwa mbele, Motorola One Macro inakuja na kamera ya megapixel 8 yenye uwezo wa kuchukua video hadi pixel 1080p@30.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot

Kampuni ya Motorola Yazindua Simu Mpya ya Moto One Micro

Simu hii inaendeshwa na processor ya Mediatek Helio P70 chipset inayo saidiwa na RAM hadi GB 4 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 64. Unaweza kuongeza uhifadhi huo kwa kutumia memory card ya MicroSD, yenye uwezo wa hadi GB 512. Simu hii hutumia sehemu ya memory card iliyopo sambamba na sehemu ya SIM au Line hivyo unaweza kuchagua kati ya kuweka line mbili au line moja na memory card. Sifa nyingine za Motorola One Micro ni kama zifuatazo.

Sifa za Motorola One Micro

 • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.21 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1600 pixels.
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (4×2.0 GHz Cortex-A73 & 4×2.0 GHz Cortex-A53).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Mediatek MT6771 Helio P70 (12nm).
 • Uwezo wa GPU – Mali-G72 MP3.
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
 • Ukubwa wa RAM – GB 4
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 8.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/2.0, 1/3.1″, 1.12µm, PDAF, Laser AF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.2, 1/5″, 1.75µm (dedicated macro camera), na kamera ya mwisho ni Megapixel 2 yenye f/2.2, 1/5″, 1.75µm, depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED Flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4000 mAh.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2 na GPS ya A-GPS. USB ya 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Space Blue.
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Hybrid Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Kwa Nyuma).

Bei ya Motorola One Micro

Kwa mujibu wa Motorola, simu hii imezinduliwa kwanza kwa nchini India na itakuwa inapatikana kupitia soko la mtandaoni la Flipkart kuanzia Octoba 12 kwa Rupee ya india INR9,999 ambayo ni sawa na takribani Shilingi za Tanzania TZS 324,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

Kampuni ya Nokia Kubadilisha Logo Yake ya "NOKIA"

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment