in

Samsung Yazindua Laptop Mpya Zinazofanana na Macbook Pro

Laptop hizo ni Notebook 7 ya inch 13 na Notebook 7 ya Inch 15

Samsung Yazindua Laptop Mpya Zinazofanana na Macbook Pro

Wakati ikiwa yamebaki masaa kadhaa hadi kuanza kwa mkutano wa Apple WWDC, Samsung imetumia wakati huo kuzindua laptop zake mpya za Notebook ya Inch 13 na Inch 15 ambazo zinafanana kabisa na laptop za Macbook Pro.

Kama wewe ni mpenzi wa laptop za Macbook Pro lakini huna pesa ya kutosha kununua laptop hizo, basi laptop hizi mpya za Samsung zitakupa uwezo wa kuona kama vile unamiliki laptop hizo za Apple. Kuanzia keyboard, muundo wa kioo, mpaka kava la laptop, hiyo vyote vinafanana kabisa na Macbook Pro.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Samsung Yazindua Laptop Mpya Zinazofanana na Macbook Pro

Tofauti na laptop za Apple, laptop hizi zilizopewa majina ya Notebook 7 kwa laptop yenye inch 13, zinakuja na sehemu zaidi za kuchomeka vitu mbalimbali kama vile sehemu tatu za USB 3.0, sehemu moja ya USB-C, sehemu moja ya HDMI, na sehemu moja ya kuchomeka microSD. Kama unavyojua laptop za Apple hazina sehemu hizi na unalazimika kutumia kifaa maalum (Dongle) ili kuweza kutumia sehemu hizo.

Kwa upande wa sifa, Notebook 7 inakuja na kioo cha inch 13 chenye resolution ya hadi pixel 1920 x 1080, huku ikiendeshwa na processor ya Intel Core i7-8565U ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 16. Vile vile laptop hiyo inakuja na Graphics ya Intel UHD Graphics au Nvidia GeForce MX 250 ambayo ipo sambamba na SSD ya hadi GB 512. Pia laptop hizi zinakuja na sehemu ya kuchomeka headphone pamoja na sehemu ya ulinzi ya Fingerprint (alama ya blue iliyopo kwenye kibonyezo cha keyboard).

Kwa upande wa Notebook 7 yenye inch 15 yenyewe pia inakuja na sifa zinazo fanana kabisa na ile ya inch 13, tofauti pekee iliyopo ni ukubwa wa kioo.

Samsung Yazindua Laptop Mpya Zinazofanana na Macbook Pro

Hata hivyo, Samsung ilizindua toleo la tatu la ziada ambalo ni maalum kwa wabunifu wa michoro (graphics) pamoja na wapenzi wa Game. Laptop hiyo ambayo inaitwa Notebook 7 Force inakuja kwa rangi nyeusi na inakuja ikiwa na utofauti wa graphics ya Nvidia GeForce GTX 1650.

Samsung Yazindua Laptop Mpya Zinazofanana na Macbook Pro

Kwa mujibu wa tovuti ya Laptop Mag, Laptop zote hizi zinasemekana kutegemewa kuingia sokoni kuanzia tarehe 26 mwezi huu na bei yake itategema kuanzia dollar ya marekani $999 sawa na Tsh 2,297,000 bila kodi kwa toleo la Notebook ya inch 13. Toleo la inch 15 litauzwa kwa dollar $1,099 ambayo ni sawa na takribani Tsh 2,526,000 bila kodi. Toleo la Notebook 7 Force yenye inch 15 yenyewe inategemewa kuuzwa kwa dollar $1,499 ambayo ni sawa na Tsh 3,445,000 bila kodi.

Kumbuka bei hizo zinaweza kubadilika kutokana na kodi au kupanda na kushuka kwa viwango vya kubadilisha fedha.

Laptop za Mwaka 2021 Ambazo ni Bora Kwa Matumizi 2023

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment