Mara nyingi watu wamekuwa wakiniuliza nini faida ya kutengeneza website na unapataje faida au pesa, vilevile pia watu wengi wamekuwa na maswali kuhusu njia za kupata faida kwa kuwa na website au kuwa na application.
Sasa leo naenda kukuletea makala ambayo nadhani kwa namna moja ama nyingine itakuwa ni msaada kwako na itaweza kufungua dunia na kukupa msaada wa jinsi unavyoweza kuanza biashara mtandaoni. Nakushauri usome makala nzima kwani hapa utaweza kupata maujanja mbalimbali ikiwa pamoja na njia ambazo sisi tunazitumia kuweza kupata pesa mtandaoni.
TABLE OF CONTENTS
Utangulizi
Kwanza nianze kwa kuwakaribisha wote lakini kama zilivyo makala nyingine kwenye tovuti ya Tanzania Tech hii nayo sio makala ambayo itakuwa ni kwa ajili ya kila mtu. Kama wewe unatafuta njia rahisi ya kutengeneza pesa mtandaoni basi nakushauri usipoteze muda kwenye makala hii, zipo makala nyingi hapa Tanzania Tech ambazo unaweza kusoma na ukaweza kutengeza pesa mtandaoni kwa haraka na kwa urahisi zaidi.
Lakini kama uko tayari kufanya kazi hii kwa bidii na kama uko tayari kulipa baadhi ya gharama za kuanzisha biashara mtandaoni basi endelea kusoma makala hii kwani na kuhakikishia utapata madini ambayo na uhakika yataweza ku-kusaidia kuanza au kuendelea na biashara yako na huenda ikakusaidia kupata pesa kupitia website au application.
Biashara za Mtandaoni ni Kama Biashara Nyingine
Kwanza napenda nikwambie, kuanzisha biashara mtandaoni ni sawa na kuanzisha biashara nyingine yoyote kwani unahitaji mtaji kama biashara nyingine, unahitaji nidhamu na pia unahitaji uvumilivu kama biashara nyingine. Utofauti wa biashara za mtandaoni ni kwamba unaweza kuanza na ulichonacho hata kama ni Tsh 5000.
Wakati wa Kuanza Biashara Mtandaoni
Kwa watu wengi biashara ya mtandaoni inakuja kama biashara ya ziada, lakini ni muhimu kujua kuwa ili kufanya biashara hii unatakiwa kuweka muda wako sawa kwa asilimia 100 tena hasa pale biashara yako inapofikia awamu ya kuchipua. Ukweli ni kuwa, kama wewe ni mtu mwenye kazi inayokubana au familia yako inakubana sana kwa namna yoyote basi biashara mtandaoni hitakuwa na changamoto kubwa kwako, hii ni kwa sababu huku mtandaoni kuna mabadiliko ya kila mara hivyo inakubidi na wewe kubadilika kila mara na kama ukishindwa kubadilika kutokana na ubize na mambo mengine, basi hutoweza kupata nafasi ya kupata wateja pamoja na kuendana kasi ya mabadiliko ya biashara za mtandaoni.
Unachotakiwa kufanya ni kuweka muda wako kwenye biashara yako kwa angalau asilimia 70 hasa pale unapoanza na nyingine 30 hakikisha unaziweka pale unapofikia hatua ya kuchipukia. Kama unapesa za mtaji unaweza kumuajiri mtu wa kufanya kazi muda wote, lakini pia hii inategemeana na aina ya biashara kwani biashara nyingine unaweza kuzifanya hata kama uko bize na mambo mengine.
Jinsi ya Kuchagua Biashara Sahihi ya Mtandaoni
Mara nyingi binadamu tunakuwa na matamanio, kama ukiona mtu mwingine amefanikiwa mtandaoni kwa kufanya kitu fulani na wewe unataka kufanya hicho hicho, ijapo kuwa wapo watu waliofanikiwa kwa njia hii lakini ukweli watu wengi hukata tamaa hasa pale mambo yanapokuwa magumu zaidi, Hivyo hii sio njia sahihi hasa kwa wewe unaetaka kuanzisha biashara mtandaoni.
Kitu cha muhimu cha kufanya ni kuangalia kitu unachokipenda wazungu wanasema “Follow your own passion—not your parents’, not your teachers’—yours.” hii ikiwa na maana “Fuata kitu kinacho kupa wewe shauku, sio kitu alichokwambia mzazi wako au mwalimu wako”.
Msemo huo unamaana sana kwenye biashara na sio kwenye biashara za mtandaoni pekee, kifupi ni kuwa “akili za kupewa ongezea na za kwako”. Kuna mambo mengi sana ambayo hayajafanywa mtandaoni tena hasa hapa Tanzania, hivyo kumbuka hicho kitu unacho kipenda unaweza kukifanyia kazi na kikapendwa na watu hapa Tanzania na dunia kwa ujumla na huenda baadae kita kutengenezea pesa na kukupa faida kuliko ulivyo tegemea. Muhimu ni kufuata ndoto zako haijalishi ndoto zako ni kubwa au ni ndogo kiasi gani.
Mtaji wa Pesa ni Muhimu lakini Sio Muhimu Sana
Ni ukweli usio pingika kwenye kila hatua ya kutaka kuanzisha biashara ni lazima kuwa na mtaji wa pesa taslimu, lakini kuna baadhi ya biashara kuwa na vifaa fulani ni muhimu kuliko hata kuwa na pesa taslim. Kwenye biashara ya mtandaoni ni muhimu sana kuwa na nyenzo ambazo zitakuwezesha kuwepo mtandaoni, hapa nina maanisha angalau uwe na kompyuta, pia uwe na simu janja au smartphone, vifaa hivi ni muhimu sana kuwa navyo kwani ndio mtaji wenyewe.
Najua utakuwa unasema sasa hii si ndio pesa yenyewe..!, lakini kuondoa hayo mawazo labda ni kwambie haijalishi unatumia kompyuta ya aina gani, au simu ya aina gani, ili kuanza biashara mtandaoni cha muhimu ni kuanza haijalishi laptop yako haikai na chaji au simu yako imepasuka kioo ukiwa na kifaa cha aina yoyote kati ya hivyo basi unaweza kuanza kufanya biashara mtandaoni.
Siri ni kuwa hata mimi binafsi nilianza na laptop ambayo inazima yenyewe bila sababu, yani uko katikati ya kazi au unaandika makala basi unashangaa laptop imezima na kazi imepotea. So nilikuwa na save kila sentensi ninayo andika.. anyway na ilikuwa inanichukua karibia lisaa kuandika makala moja tu…, huko ndipo mimi nilipoanzia hivyo wewe pia usijalishe unaanza vipi bali cha msingi ni kuanza na utakuja kuona mafanikio baadae na huto amini kama ulikuwa hapo miezi kadhaa iliyopita.
Pesa ya Mtandaoni Huja Baadae
Mara nyingi watu wanaotaka kufanya biashara mtandaoni huwa na mawazo ya pesa za haraka haraka, lakini labda ni kwambie siri, kwenye biashara ya mtandaoni pesa ni kitu ambacho utakipata baadae tena muda huwa mrefu kama biashara yako ni tofauti au ambayo haijazoeleka na watanzania kama unalenga soko la watanzania.
Kitu cha muhimu ni kuhakikisha unafanya kazi nzuri kwanza na baadae kazi yako itakapo onekana ndipo utatengeneza kipato tena kinacho eleweka. Unachotakiwa kujua ni kuwa kufanya biashara mtandaoni ni kama kuwa mwalimu au kuwarahishia watu kupata wanachokitaka, na endapo watu hawa watahitaji zaidi kuliko vile unavyowapa basi hapo ndio utaweza kutengeneza pesa kwa kutoza pesa kwenye kile unachofanya.
Biashara ni nyingi mtandaoni lakini mara nyingi biashara za bure ndizo zinazofanikiwa sana, Ukiangalia Google inategeneza trilioni ya pesa na karibia huduma zao zote ni za bure kutumia, je huoni kwamba hiyo ndio njia sahihi ya kufanya biashara mtandaoni. Kitu cha muhimu ni kupata watu wengi zaidi alafu pesa itakuja yenyewe baadae.
Sasa hapa ndipo mahali ambapo najua wengi watasoma, ukweli mimi binafsi nimeanza biashara mtandaoni siku nyingi sana na baadhi ya biashara tayari zimefanikiwa kunipa kupato cha kuweza kuendesha maisha yangu ya kila siku. Kwa mfano moja ya website ambazo nina miliki zimefanikiwa kuingiza kiasi cha Tsh za kitanzania milioni 20 na kuendelea, unaweza kuona ushahidi hapo chini.
Sidhani kama kuna haja sana ya kuongelea hizi namba ila ukweli ni kwamba kwenye baadhi tu ya tovuti ambazo zinafanya kazi hicho ndio kiwango cha pesa unacho tegemea ndani ya miezi minne tu. So kama unavyoweza kuona kuanza biashara mtandaoni ni kitu kigumu na pia nirahisi kama utakuwa unapenda unacho kifanya, pia usione kitu fulani kimefanikiwa ukadhani ni rahisi kufika hapo unahitaji muda, ubunifu na subira kwa kiwango kikubwa sana.
Nachoweza kukusaidia ni kukuonyesha njia hivyo basi, binafsi natangaza kuwa Tanzania Tech tumekubaliwa kuanzisha njia za kuwasaidia watu kupata pesa mtandaoni kupitia Apps pamoja na website. Hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech ili uwe wa kwanza pale jambo hili litakapo tangazwa. Mpaka wakati mwingine pole kwa maneno mengi lakini natumaini yatakusaidia.
Hivi nijinsi gani una weza kuunga application kwenye loptop
ni nia gani ya kutengeneza application hatua kwa hatua mwanzo mpaka mwsho
Asante mzidi tu kutupa update za teknolojia punde zitokapo
Karibu sana.
Ni kiasi gani cha fedha kinachofaa kufungua Website
Inategemea na aina ya website