in

Jaribu Game Bora za Mpira Kwenye Simu ya Android (2019)

Jaribu Game hizi bora za Mpira kwenye Simu yako ya Android

Jaribu Game Bora za Mpira Kwenye Simu ya Android (2019)

Najua ni watu wengi wanapenda mpira wa miguu na kutokana na sikukuu zinazokuja najua utakua nyumbani hivyo, hizi hapa Game za mpira ambazo unaweza kucheza kwenye simu yako ya Android na Game hizi n moja kati ya game bora sana hivyo endelea kusoma makala hii mpaka mwisho kama wewe n mpenzi wa mpira wa miguu.

  •  PES 2018 Pro Evolution Soccer
eFootball™ 2024
Price: Free

PES ni moja kati ya game maarufu sana kwa wapenzi wa game za mpira game hii inamuonekano mzuri na ina hususha wachezaji maarufu, kama ulikuwa unatauta game bora ya kupoteza muda siku hii ya sikukuu basi game hii ni bora sana kwako.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Dream League Soccer 2018
Dream League Soccer
Price: To be announced

Tofauti na game nyingine Dream League 2018 ni game ya aina yake kwani game hii inakuruhusu kuweza kuongoza timu yako hii ikiwa na kuuza wachezaji kununua pamoja na kuongeza kiwango kwa kucheza mechi mbalimbali. Game hii inakuruhusu kuhifadhi data ambapo unaweza kucheza pale utakapo ishia kila mara utakapo taka.

  • FIFA Soccer

Haiwezekani kuandika game bora za Android na kusahau game hii ya FIFA, Game hii ni moja kati ya game nzuri sana na ni game ambayo ina sehemu nyingi kuliko game nyingine zote kwenye list hii. Kwa kutumia game hii unaweza kutengeneza kikosi cha timu unayoipenda na kukiongoza ikiwa pamoja na kununua wachezaji kuuza na mengine mengi. Kingine ni kuwa unaweza kucheza na timu ya watu wengine live kupitia internet.

  • Real Football
Real Football
Price: Free

Real Football ni game nyingine ya Android ambayo ni bora game hii itakupa uwezo wa kufanya mambo mbalimbali ikiwa pamoja na kufundisha wachezaji, kubadilisha viwanja mbalimbali kama unavyotaka pamoja na kuchati na marafiki mbalimbali wanayotumia game hiyo duniani.

  • Score! Hero
Score! Hero
Price: Free

Score! Hero ni game ambayo ni tofauti sana, game hii inahusu mchezaji ambaye ni mchanga na ambaye anataka kuwa mchezaji mkubwa na ili kufika anapotaka inabidi kupitia vikwanzao mbalimbali ndani ya game hiyo. Game hii ni nzuri sana unaweza kucheza na watu mbalimbali duniani.

  • Real World Soccer League

Real World Soccer League ni moja kati ya game nzuri sana na ni moja kati ya game ambazo ni rahisi kucheza. Game hii inakupa uwezo wa kutengeneza kikosi chako pia unaweza kucheza na timu mbalimbali za kutoka nchi mbalimbali. Game hii ina muonekano mzuri sana na ukianza kucheza huto weza kuacha kuicheza.

  • Ultimate Soccer – Football

Ultimate Soccer ni game ya mwisho kwenye list hii game hii itakupa uwezo wa kutengeneza timu yako na kucheza kupitia kwenye makombe mbalimbali ya League au World Cup tournament. Game hii ni nzuri sana na game hii inakuruhusu kununua au kuuza mchezaji au hata kumuhamisha mchezaji wa timu yako.

Na hizo ndio game ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo, Game hizi zinapatikana bure kabisa kupitia Play Store unaweza kuzipakua sasa kwa kubofya game unayopendekeza na utapelekwa kwenye ukurasa wa kudownload. Kama umependa game hizi shiriki na uwapendao na kama una maoni au maswali unaweza kutuandikia kwenye maoni hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.