Jinsi ya Kuchat Kupitia App za Youtube za iOS na Android

Jifunze jinsi ya kutumia sehemu mpya kwenye Youtube
YouTube Chat YouTube Chat

Hivi karibuni youtube imeleta sehemu mpya ya share on youtube sehemu hii itakusaidia kuchati kupita programu za Android na iOS za mtandao wa youtube. Makala hii ni kwaajili ya kujifunza jinsi ya kutumia sehemu hiyo mpya.

Kama tayari umesha update app yako ya Youtube, basi moja kwa moja ingia kwenye programu yako kisha utaona sehemu mpya iliyo-ongezwa iliyo andikwa SHARE bofya hapo kisha utapelekwa kwenye uwanja mpya ambapo utaweza kuchat na kushare video.

UPDATE 2018 : Sehemu ya SHARE sasa imebadilika ni Activity hatua nyingine ni kama zilivyo.

Advertisement

Baada ya hapo bofya sehemu ya juu kabisa iliyo andikwa View Contact, kisha hapo utaona njia mbili za kualika watu ili kuweza kuchat kwenye app ya Youtube. Chagua njia unayo taka kisha chagua unayetaka kumualika kisha mtumie link ambayo hiyo ndio itasaidia mtu kuweza kujiunga na majadiliano kwenye app hizo, angalia video kujifunza zaidi.

https://www.youtube.com/watch?v=UgcEDC1FuOk

Kama utakuwa umekwama mahali usisite kutuandikia kwenye maoni hapo chini nasi tutakujibu moja kwa moja na haraka zaidi.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

8 comments
  1. Hivi karibuni, ulituhaidi simu za nokia andirod zitaingia, lakini mpaka sasa hivi nikichek kwenye maduka yetu azipatikani vpi azijafika?

    1. Hii inategemeana sanaa upatikanaji wa simu hizo, kama zimesha sambaa sana bila hivyo itakubidi usubiri kidogo.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use