in

Sasa Chat na Share Video Moja kwa Moja Kwenye App ya YouTube

Sehemu ya kuchat na kushare video youtube sasa imewezeshwa

Sasa Chat na Share Video Moja kwa Moja Kwenye App ya YouTube

Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti yetu lazima utakuwa umesha soma makala iliyokuwa inagusia kuhusu kuja kwa sehemu ya kuchat na kushare video kwenye Youtube.

Kama ulisha soma makala hiyo basi hii ni habari njema kwani sasa sehemu hiyo imewezeshwa rasmi na Youtube na sasa utaweza kuchati na watu wengine huku mkiongelea video mbalimbali kupitia programu za youtube za iOS na Android.

Sehemu hiyo inapatikana kwenye app zote ikiwa imeandikwa share, kama bado ujaiona sehemu hiyo basi hakikisha una update programu yako ya Youtube na utaweza kuanza kuchati na kushiri video na watu mbalimbali kupitia mtandao wa Youtube.

Mbali na kushare pamoja na kuchat kuhusu video, vilevile utaweza ku-like chat za mtu kupitia app hiyo moja kwa moja ikiwa pamoja na kualika watu mbalimbali, ili kualika watu kwenye chat zako pamoja na jinsi ya kutumia sehemu hiyo mpya endelea kutembelea Tanzania Tech.

UPDATE : Kama unataka kujifunza jinsi ya kutumia sehemu hii bofya hapa

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Hizi Hapa Apps Kwaajili ya Wanachuo Mwaka wa Kwanza

Chanzo : Daily Mail

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.