in

Tukumbushane : Sheria za Makosa ya Mitandaoni na Adhabu Zake

Kama umeshau kidogo sheria za makosa ya mitandaoni basi soma hii

Makosa ya Mtandaon

Hivi karibuni kumekua na mijadala mbalimbali kuhusu sheria za makosa ya mtandaoni, sheria ambazo zilitungwa na kupitishwa na bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania hapo mwaka 2015, lakini sheria hizi ni watu wachache sana wanazijua au wanajua mahali pakuzi pata ili kuweza kuzisoma basi leo Tanzania Tech tunakuletea makala hii ya sheria hizo na adhabu zake.

Kwa mujibu wa blog ya michuzi blog mambo yafuatayo ndio baadhi ya mambo muhimu ambayo ni muhimu kuyajua kama unataka kuwa salama na kujiweka mbali na adhabu inayotokana na makosa ya mtandaoni.

Install Android App
Price: Free
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Nyimbo Mpya Screenshot
 • Epuka Kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii yetu kupitia mitandao.
 • Epuka Kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza
  kupelekea kuvuruga amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao.
 • Epuka Kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao mbalimbali ( Whatsapp, Facebook, YouTube, Instagram n.k ).
 • Epuka Kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii.
 • Epuka Kushiriki kusambaza chochote kati ya vilivyotajwa hapo juu (kutuma kama ulivyopokea) itakugharimu.
 • Epuka Wizi kupitia mitandao mbalimbali na mitandao ya simu utakugharimu.
 • Epuka Kumpatia mtu line yako ya simu na kutumika kufanyia wizi ama utapeli itakugharimu.
 • Epuka Kushiriki kumchafua mtu,taasisi,kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao pia itakugharimu.
 • Epuka Kupoteza simu bila kutoa taarifa na kufunga mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kutumika kufanya uhalifu na ukaangukia hatarini.
 • Epuka Kutumia mtandao kwa utapeli kupitia ‘brand’ ama jina la mtu itakugharimu.

Hayo ni baadhi ya mambo tu ambayo ni muhimu sana kuzingatia sana kwenye sheria za makosa ya mitandao, kusoma sheria zote kamili na adhabu zake unaweza kudownload sheria hizo zilizoko kwenye mfumo wa pdf hapo chini, sheria hizo zipo kwa kiswahili na kingereza kiswahili kipo mwisho kabisa wa document au hati hiyo.

SHERIA ZA MAKOSA YA MTANDAONI

Bila shaka utakuwa upata kujua au kujikumbusha baadhi ya sheria ambazo kwa namna moja ama nyingine ulkua umesahau, kama una swali au maoni unaweza kutuandikia hapo chini.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : Mst.go.tz, Michuzi Blog

Amani Joseph

Tukumbushane : Sheria za Makosa ya Mitandaoni na Adhabu Zake

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Mfumo wa iOS 17 Kupatikana Rasmi September 18 (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

15 Comments