Jinsi ya Kutumia Smartphone Yako Kama Modem Kwenye PC

Jinsi ya Kutumia Smartphone Yako Kama Modem Kwenye PC Jinsi ya Kutumia Smartphone Yako Kama Modem Kwenye PC

Tecknolojia kwasasa imerahisisha sana maisha iwe una smartphone au una tablet lazima kwa namna moja ama nyingine utakua kuna urahisi flani unaoupata kutokana na kuwa na simu yako au tablet, leo hii nitawaonyesha namna nyingine rahisi kabisa ya kugeuza simu yako kuwa modem ili undelee kurahisisha maisha yako na kufurahia kuwa na hiyo smartphone yako au tablet.

Oky! moja kwa moja tuanze somo hili rahisi kabisa kumbuka kwa leo nitawafundisha kwa kupitia simu yako yenye uwezo wa Android, unachoitaji cha muhimu kwa somo hili ni waya wa simu yako yani USB pia hakikisha simu yako imewezeshwa au imewashwa internet data.

Advertisement

Hatua ya kwanza chomeka waya wa USB kwenye simu yako kisha chomeka kwenye pc yako kisha baada ya hapo kama ndo unachomeka simu yako kwa mara ya kwanza kwenye PC acha mpaka imalize ku-install driver au viunganish maalumu kwenye Computer yako.

Hatua ya pili nenda kwenye “Menu” ya simu yako ambayo kawaida kwenye simu nyingi inakua vidoti kama vinne au zaidi, kisha chagua “Settings” alafu kama unatumia Samsung au Sony nenda kwenye sehemu iliyoandikwa “More” sehemu hii upatikana sana kwenye simu zenye uwezo Android, baada ya hapo sogea chini kidogo utaona maandish yameandikwa “Tethering and Hotspot” pia kumbuka haya maneno hua mara nyingi yafanana kwenye simu nyingi zenye mfumo wa Android.

Kisha hatua ya tatu baada ya kuchagua maneno hayo hapo juu utaletwa moja kwa moja kwenye menu ambayo kama utakua umechomeka simu yako kwenye computer kwa kutumia USB sehemu hii itaonekana kama hauja chomeka simu yako sehemu hii itafifia ikiwa na maana kuwa sehemu hii hufanya kazi ukiwa umeunganisha simu yako kwa kutumia USB waya.

Weka on au bofya sehemu iliandikwa “USB Tethering” kisha utaona alama imetokea juu kwenye notification panel ikiwa inaonyesha kwamba umewezesha simu yako kutumia internet kwa waya au “USB Tethering” kufikia hapo utaona kwenye computer yako iki-install driver tena kwa mara nyingine acha mpaka imalize kisha baada ya hapo utaona Computer yako imewezeshwa na internet.

Kama kawaida ya tanzania tech kama unataka kujifunza kwa vitendo video hiyo hapo juu ni kwaajili yako usisahau ku-comment kama unataka maelekezo zaidi.

13 comments
  1. da! nimekupata sana ngoja nijalibu kuchomeka kwenye lap top yangu aiseeee huwa namaindi sana kutumia hiyo njia ila nilikuwa nashindwa kuunganisha da!

  2. Mbona m cm yangu nikichomeka usbKweny labtop uwa inachaji tu na Yale maandishi ya kuonesha usb connected ayatokei/!! Iv tatizo nn??

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use