super-mario-run

Game ya Super Mario Yaja kwenye iPhone 7 na Android

Wapenzi wa gemu siku ya tarehe 7 walifurahi sana kutokana na kutangazwa kwa kuja kwa game ya Super Mario Run kwenye simu mpya ya iPhone 7 pamoja na simu nyingine za Apple (ikiwemo iPads), Hata hivyo wapenzi wa game hiyo kote duniani walionakana kukata tamaa kutokana na game hiyo kuja kwenye simu za Apple pekee.

Hata hivyo habari kutoka kwenye blog ya teknolojia ya nchini marekani ya 9to5google iliandika kuwa sasa imepata udhibitisho kamili ya kuwa gemu hiyo ya super mario run itakuja pia kwenye simu zenye mfumo wa Android.

Kwa wale wasio ijua game ya super mario ni game ya siku nyingi ambayo ilikuwa kwenye mfumo wa zamani wa game za nintendo au (Game Boy) kwa wale wanaoifuhamu zaidi. Hata hivyo bado haijajulikana kuwa ni lini game hiyo itakuja rasmi kwenye Android lakini kwenye iOS kaa tayari kucheza game hii mwezi december mwaka huu.

Kama unataka kupata habari za game hii pindi itakapo toka endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
iphone 7
Yakujua Kabla ya Kununua Simu Mpya ya iPhone 7
Next Post
instagram-ya-kibiashara

Jinsi ya Kubadilisha Instagram Kuwa ya Kibiashara