Sasa Unaweza Kutengenza Muziki Kupitia Google Gemini

Unaweza kupakia picha au video na kuiomba Gemini itumie maudhui hayo kutunga wimbo
Sasa Unaweza Kutengenza Muziki Kupitia Google Gemini Sasa Unaweza Kutengenza Muziki Kupitia Google Gemini

Google imepiga hatua nyingine kubwa katika ulimwengu wa Akili Mnemba (AI) kwa kuleta uwezo wa kutengeneza muziki moja kwa moja kupitia programu ya Gemini. Kwa kutumia mfumo wa Lyria 3 uliotengenezwa na Google DeepMind, watumiaji sasa wanaweza kubadilisha mawazo yao au picha kuwa nyimbo kamili za sekunde 30.

Advertisement

Sifa na Uwezo wa Lyria 3 Ndani ya Gemini

Mfumo huu mpya umeboreshwa kwa kiasi kikubwa na unatoa uwezo wa kipekee kwa watumiaji:

  • Kutunga Mashairi Moja kwa Moja: Huhitaji tena kuumiza kichwa kuandika mistari ya wimbo. Lyria 3 inajiandikia mashairi yenyewe kulingana na maelezo unayoyatoa.
  • Udhibiti wa Kibunifu (Creative Control): Una uwezo wa kuchagua mtindo wa muziki, aina ya sauti (vocals), na kasi ya mdundo (tempo). Kwa mfano, unaweza kuielekeza Gemini itengeneze wimbo wenye mahadhi ya Bongo Flava, unaoelezea hadithi au kumbukumbu fulani, na itafanya hivyo kwa sekunde chache.
  • Kutoka Kwenye Picha Hadi Wimbo: Sio maandishi pekee; unaweza kupakia picha au video na kuiomba Gemini itumie maudhui hayo kutunga wimbo ambao mashairi yake yanaendana na hisia za picha husika.
  • Kasha la Wimbo (Cover Art): Kila wimbo wa sekunde 30 unaotengenezwa unaambatana na picha maalum ya kasha iliyotengenezwa na mfumo wa Nano Banana, ikirahisisha kusambaza (sharing) kwa marafiki.

Mfano wa Nyimbo

Hii hapa no mfano wa nyimbo ambayo tumejaribu kutengeneza kwa kutumia Gemini, unaweza kusikia maadhi ya nyimbo kwa kusikiliza nyimbo hapo chini.

Usalama na Uhakiki wa Maudhui (SynthID)

Ili kukabiliana na changamoto za hakimiliki na utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa na AI, Google imeweka mfumo wa SynthID kwenye nyimbo zote zinazozalishwa na Gemini. Hii ni watermark isiyosikika kwa masikio ya kawaida ambayo inathibitisha kuwa sauti hiyo imetengenezwa na AI ya Google.

Pia, Gemini ina uwezo wa kuhakiki nyimbo kama imetengenezwa na AI au la. Kwenye suala la hakimiliki, mfumo huu umeundwa kuleta ubunifu mpya na sio kuiga wasanii waliopo. Ukitaja jina la msanii fulani, Gemini itatumia tu mtindo huo kama hamasa (inspiration) badala ya kunakili sauti yake moja kwa moja.

Upatikanaji Wake

Kipengele hiki cha Muziki Kupitia Gemini kinapatikana katika toleo la majaribio (beta) kwenye programu ya Gemini kwa watumiaji wenye umri kuanzia miaka 18+. Kwa sasa inasaidia lugha kadhaa ikiwemo Kiingereza, Kijerumani, Kihispania, Kifaransa, na nyinginezo. Watumiaji wenye vifurushi vya Google AI Plus, Pro, na Ultra watapata kiwango kikubwa zaidi cha matumizi, na pia mfumo huu unaanza kupatikana kwa watengeneza maudhui wa YouTube kupitia “Dream Track”.

Hitimisho

Ujio wa Lyria 3 kwenye Gemini unalenga kuwapa watu njia mpya na ya kufurahisha ya kujieleza kupitia muziki wa kipekee katika maisha yao ya kila siku. Iwe ni kwa ajili ya kutengeneza wimbo mfupi wa kufurahisha marafiki au kuweka vionjo kwenye video za YouTube Shorts, mfumo huu unafungua milango mipya ya ubunifu wa sauti unaoongozwa na AI.

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *