Tumia Aina Mbalimbali za AI Kama ChatGPT Kwa Wakati Moja 1

Tumia Aina Mbalimbali za AI Kama ChatGPT Kwa Wakati Moja

Katika ulimwengu wa AI ni wazi kuwa zipo aina mbalimbali za AI Chat Bots au Language Model ambazo pengine inawezekana ulikuwa huzijui.

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia mpya na rahisi ya kutumia AI kama ChatGPT na nyingine nyingi kwa pamoja na kwa urahisi. Njia hii ni rahisi na huitaji kupakua programu nyingi kwa kwenye simu yako au kifaa chochote unachotumia.

Kupitia njia hii utaweza kutumia mifumo ya AI kama ChatGPT, Poe, Midjonery na nyingine nyingi. Bila kuinstall programu tofauti kwa kila AI.

Tumia Aina Mbalimbali za AI Kama ChatGPT Kwa Wakati Moja 2

Kwa kuanza unaweza kutembelea tovuti hapo chini, na moja kwa moja unaweza kujisajili na kuchagua aina ya AI unayotaka kutumia au Unaweza kupakua programu za iOS au Android.

Tembelea Tovuti Hapa

Kama unataka urahisi unaweza kudownload app za Android na iOS ya mfumo huu ambayo inapatikana kwenye masoko yote.

Kwa Watumiaji wa Android

Kwa Watumiaji wa iOS

Poe – Fast AI Chat
Price: Free+

Unaweza kujisajili kwa kutumia akaunti yako ya Google kwa ajili ya kurahisisha matumizi, ikiwa pamoja na kulogin bila kutumia password.

Baada ya kutengeneza akaunti unaweza kuendelea kutumia bots za aina mbalimbali kwa urahisi kupitia simu yako au kompyuta.

Kama unataka kuendelea kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu mifumo ya akili bandia yaani AI hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech pia hakikisha unapakua app ya Tanzania Tech ili kupata maujanja kwa urahisi zaidi.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Camera za Simu za TECNO Sasa Kuchukua Rangi Halisi ya Ngozi 3
Camera za Simu za TECNO Sasa Kuchukua Rangi Halisi ya Ngozi
Next Post
Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube 4

Jinsi ya Kupunguza Matumizi ya Bando Kupitia YouTube