Hivi majuzi instagram ilitoa toleo lake jipya ambapo sasa application hiyo imekuja na muonekano mpya kabisa ikiwa imebadilika kuanzia picha ya programu hiyo pamoja na muonekano mzima wa programu hiyo, wataalamu wa mambo ya programu duniani kote wamesema kuwa muonekano huo mpya umefanya instagram kuonekana kama vile ni programu mpya kabisa.
“Ikiwa imebadilika rangi pamoja na picha ya programu hiyo bado iko kama zamani lakini kwa watu wapya ni kama vile ni programu mpya kabisa kutokana na muonekano, kweli inaonekana kama ni programu mpya kabisa tofauti na awali tulivyo zoea”, alisema mtaalamu kutoka katika blog ya techcruch ya nchini marekani.
Kama bado ujaipata instagram yenye muonekano mpya nenda sasa kwenye Play Store na Update utaona instagram mpya yenye muonekano mpya kabisa.

