Instagram imetangaza kuwa inafanyia majaribio sehemu mpya ya video kwenye mtandao huo itwao Features, ambao watumiaji wataruhusu watumiaji kupakia video za mlalo zenye urefu wa hadi dakika 90.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka The Hollywood Reporter, majaribio hayo yalianza siku ya Jumatatu na kwa sasa yanawahusu wazalishaji maudhui wachache walioteuliwa nchini Marekani.
Hata hivyo, ripoti hiyo imeongeza kuwa Instagram tayari ilikuwa ikifanyia majaribio kipengele hicho na wazalishaji maudhui nchini Brazil.

Makamu wa Rais wa Bidhaa wa Instagram, Tessa Lyons, pamoja na mkuu wa mtandao huo Adam Mosseri pia wameshiriki maelezo zaidi kuhusu mfumo huo mpya wa video ndefu. Kipengele hiki kinalenga zaidi waandaaji wa podcast, kikiwaruhusu kushiriki vipindi vyao kamili au vipande virefu zaidi vya video kwenye mtandao huo.
Hapo mwanzo, video hizo ndefu zitaonyeshwa kama klipu fupi kwenye sehemu ya Explore. Kisha Watazamaji wanaweza kubofya kitufe kipya cha ‘Tazama video kamili’ kwenye klipu hiyo ili kuanza kutazama video yote.
Features itaanza kupatikana kwanza kwenye programu ya simu ya Instagram, huku uwezo wa kutumika kwenye programu ya Instagram kwa ajili ya TV ukipangwa kuja hapo baadaye. Mfumo huu mpya wa video ndefu unatarajiwa kuwafikia watumiaji wote nchini Marekani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu au mapema mwaka ujao.