Apple Imethibitisha Kuwepo Kwa Tatizo Simu za iPhone Duo 1

Apple Imethibitisha Kuwepo Kwa Tatizo Simu za iPhone Duo

Tunatambua uwepo wa tatizo linaloathiri kioo cha ndani kwenye idadi ndogo ya simu za iPhone Duo

Kampuni ya Apple imejibu ripoti kuhusiana na kuwepo kwa tatizo la kupasuka kwa kioo cha ndani cha iPhone Duo. Katika taarifa kwa 9to5Mac, kampuni hiyo imekiri kuwa inatambua tatizo hilo na imetoa ushauri wa msingi.

Apple Imethibitisha Kuwepo Kwa Tatizo Simu za iPhone Duo 2

Apple ilituma taarifa ifuatayo kama majibu wa tovuti ya 9to5Mac

“Mapokezi ya iPhone Duo kutoka kwa watumiaji wa awali yamekuwa mazuri sana, na tunaona mambo ya kusisimua kutoka kwa waendelezaji programu ambao wanaboresha programu zao kwa haraka ili kutumia muundo wake wa kipekee. Tunatambua uwepo wa tatizo linaloathiri kioo cha ndani kwenye idadi ndogo ya simu za iPhone Duo. Kama watumiaji watapata matatizo na kioo cha iPhone Duo yao, wanapaswa kuwasiliana na AppleCare kwa ajili ya kubadilishiwa simu nyingine.” Imesema sehemu ya Taarifa hiyo.

Hapo Jana, kulizuka ripoti nyingi kuhusu tatizo hilo ambalo lilianza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya intaneti. Wanunuzi wa iPhone Duo wameandika na kulalamikia kuwa simu hizo kuharibika kwa haraka kwa kioo cha ndani kwenye simu zao mpya, jambo ambalo linaonekana kusababishwa na ugumu pale mtu anapotaka kufungua simu hizo ili kutumia kioo cha ndani.

Hali hii ilisababisha sauti ya mlio kusikika kutoka kwenye bawaba, na kioo kuharibika mara moja baada ya hapo.

Apple haikutoa maelezo yoyote kuhusu nini hasa chanzo chake, lakini jambo hilo halishangazi sana. Apple inadai kuwa tatizo hili linaathiri idadi ndogo tu ya simu hizo, jambo ambalo linaonekana inawezekani ni kweli ukizingatia makadirio ya mauzo ya simu hizo ambayo ni madogo.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Xiaomi Yazindua Redmi Note 17 Titan Max Yenye Ubora Zaidi 3
Xiaomi Yazindua Redmi Note 17 Titan Max Yenye Ubora Zaidi