game kiswahili

Jaribu kucheza Game Hii Bora ya Kiswahili

Nimesha wahi kuona baadhi ya game za kitanzania zingine zilifanikiwa kufika kwenye Play Store zingine hazikufika lakini hivi karibuni kuna game moja limenifanya niweze kuandika post hii.

Game hii inaitwa Pic Pazzle game ni game nzuri sana na inakusaidia kupoteza muda na kizuri zaidi unaweza kucheza offline yani bila kutumia Internet, kingine game hii ina MB 5 tu hivyo inamwezesha mtu yoyote kuweza kuipakua kwenye simu yake.

Jaribu kucheza Game Hii Bora ya Kiswahili 1
The app was not found in the store. :-(

Kuhusu game hii unachokifanya ni kama ile michezo ya kizamani kidogo ya kuunganisha picha ili iweze kutokea yote, hakika ni mchezo wa zamani sana kwa wale wanaojua mchezo huu pia mchezo huu ni mzuri sana kwa watu wa rika zote iwe mtoto au hata mtu mzima, ukweli ni kwamba game hi ni nzuri na itakufanya uwe bize na simu yako kila mara.

Download Game hii ili kutoa sapoti kwa vitu vya nyumbani ipakue sasa iko Play store au unaweza kubofya hapo juu kui-download moja kwa moja kwenye simu yako, pia kama unataka habari mbalimbali za michezo na game mbalimbali endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa kupakua App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Simu mpya ya Iphone 7 kuzinduliwa
Angalia Hapa Uzinduzi wa Simu Mpya ya iPhone 7
Next Post
yaliyojiri-jana-kwenye-mkutano-wa-apple

Yaliyojiri Kwenye Tamasha la Uzinduzi wa Apple iPhone 7