kufata meseji fb messnger

FB Messenger Kuja na Njia ya Kurudisha Meseji Ulizo Kosea

Baada ya mtandao wa Facebook kuleta sehemu ya Delete For All kupitia App ya WhatsApp, hivi karibuni mtandao huo uko njiani kuleta sehemu mpya kupitia app yake ya Facebook Messenger itakayo kuwezesha kurudisha meseji uliyokosea kutuma.

Kama ilivyo kwenye WhatsApp,  kupitia sehemu hiyo pia itakuruhusu kufuta meseji uliyokosea kutuma ambapo meseji hiyo itafutika kwa upande wako, na pia kwa kutumia sehemu ya “unsend” meseji hiyo itaweza kufutika kwa uliyemtumia pekee.

Kupitia sehemu hiyo pia utaweza kufuta meseji ulizokosea kutoka mda machache tokea utume meseji hizo, hivyo utaweza kurudisha meseji ambazo zimekaa kwa muda mrefu sana. Kwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu lini sehemu hii itakuja kwenye App ya Messenger hivyo hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech tutakujuza zaidi kuhusu sehemu hii.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Hizi hapa sifa na bei ya Nokia 3.1 Plus
Zifahamu Hizi Hapa Sifa na Bei ya Nokia 3.1 Plus
Next Post
muonekano wa simu ya Android-launcher

App 13 za Kubadilisha Muonekano wa Simu Yako ya Android