Jinsi ya Kufuta Meseji WhatsApp na Zifutike kwa Kila Mtu

Jifunze jinsi ya kufuta meseji na itafutika kwa wote ulio watumia
kufuta meseji whatsapp kufuta meseji whatsapp

Sehemu mpya ya kufuta meseji ya WhatsApp inayoitwa Delete For Everyone imetoka rasmi lakini kuna watu wengi hawajui jinsi ya kuitumia sehemu hiyo. Yafuatayo ni maelezo jinsi ya kutumia sehemu hiyo.

Kwa kuanza ingia kwenye programu yako ya WhatsApp kisha fungua meseji unayotaka kufuta, baada ya hapo shikilia meseji unayotaka kufuta kisha chakua alama ya kufuta inayotokea upande wa kulia juu. Bofya hapo kisha utaona sehemu tatu yaani Delete for Me, Cancel na sehemu ya Delete For Everyone bofya hapo kisha malizia kwa kubonyeza OK na hapo utakuwa umefuta meseji hiyo kwa kila mtu ulie mtumia.

Advertisement

Kumbuka kuwa usipo ona sehemu hizo bosi ujue kuwa bado sehemu hiyo haijawezeshwa kwenye programu yakjo ya WhatsApp, Vilevile kumbuka kuwa una uwezo wa kufuta meseji ambazo zina muda wa dakika 7 na sio pungufu.

Na hapo utakuwa umeweza kufuta meseji za WhatsApp na zitafutika kwa kila mtu, kama unataka kujifunza maujanja zaidi unaweza Subscribe kwenye channel yetu ya Tanzania Tech kupitia kwenye mtandao wa Youtube.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use