Facebook Yaja na Valentine’s Day Cards Kwa Siku ya Wapendanao

Hivi ndivyo Facebook inavyo kusaidia kusherekea vizuri siku ya wapendanao
Facebook na Siku ya Wapendanao Facebook na Siku ya Wapendanao

Februry 14 imekaribia huu ndio wakati wa ile siku ya wapendanao inayo adhimishwa kila mwaka tarehe 14 ya mwezi wa pili, kufanya siku hiyo iwe nzuri zaidi Facebook kupitia mtandao wake wa facebook inakuletea Facebook Valentine’s Day cards, hizi ni kadi za kieletroniki ambazo utashare na mpenzi wako au watu wa karibu kwenye mtandao wa Facebook.

Kadi hizo zinategemewa kuanza kuonekana kuanzia tarehe 13 february kupitia sehemu maarufu ya News Feed. Hapo mtumiaji atapata uwezo wa kuanza kushare kadi hizo mbalimbali kupitia mtandao huo wa facebook.

Advertisement

Habari zinasema kuwa kutokana na sehemu hiyo kuonyesha kupendwa sana hapo mwaka jana, Facebook imepanga kuboresha sehemu hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza vitu vipya kwenye kadi hizo. Kumbuka sehemu hiyo siyo ya kudumu bali ni sehemu ambayo itakufanya kuongeza mapenzi mubashara kwenye siku hiyo ya wapendanao, hivyo kumbuka kutembelea mtandao wa Facebook kuanzia tarehe 13 ya mwezi February.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kuwa wa kwanza kujua yote yanayohusu teknolojia, vilevile kama wewe unataka kujua habari za teknolojia pamoja na maujanja mbalimbali kwa njia ya video basi jiunge nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube.

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *