Facebook Messenger Yaleta Group Call

Facebook Messenger Yaleta Group Call Facebook Messenger Yaleta Group Call

Kampuni ya facebook imetangaza leo kuwa imeanza kutoa toleo lake jipya la facebook messenger ambapo watu sasa wataweza kupiga simu za internet au VoIP audio kupitia magroup yao kwa kutumia programu hiyo facebook messenger.

Ili kupiga simu kwenye group lako bofya kitufe cha simu kisha chagua ni watu gani kwenye group unataka kuwasiliana nao na watapata simu yako wote kwa pamoja, pia unaweza ukaona kwenye group ni nani anaongea na nani na unaweza kuomba kujiunga nao pale watakapo kukubalia utakua na uwezo pia wa kujiunga nao, hata hivyo facebook imetangaza kuwa unaweza kupigia hadi  watu 50 tu, kama bado ujapata toleo hilo jipya usijali ndio kwanza toleo hili limetangazwa kutoka leo.

Advertisement

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *