Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kutambua Tovuti Halisi ya ESS Utumishi

Ukweli kuhusu uwepo wa Tovuti Feki za ESS Utumishi na Umuhimu wa Kutumia Tovuti Halisi
Jinsi ya Kutambua Tovuti Halisi ya ESS Utumishi Jinsi ya Kutambua Tovuti Halisi ya ESS Utumishi

ESS Utumishi, mfumo wa Employee Self Service wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni chombo muhimu sana kwa watumishi wa umma. Huwawezesha watumishi kupata taarifa za mishahara, likizo, kufanya tathmini za utendaji kazi (kupitia mifumo kama PEPMIS), na mambo mengine mengi yanayohusu utumishi wao. Kutokana na umuhimu huu, kumekuwa na ongezeko kubwa la tovuti feki (fake websites) zinazofanana au kujaribu kuiga mfumo halisi wa ESS Utumishi.

Sababu kuu za uwepo wa tovuti feki za ESS Utumishi ni:

Advertisement

Wizi wa Taarifa Binafsi (Phishing):

Wahusika wa tovuti feki huunda nakala za tovuti halisi kwa nia ya kuwalaghai watumishi kuingiza majina yao ya watumiaji (username) na nywila (password). Mara baada ya kupata taarifa hizi, wanaweza kuzitumia kupata taarifa za siri za mtumishi husika, ikiwemo taarifa za kifedha, au hata kutekeleza uhalifu mwingine.

Jinsi ya Kutambua Tovuti Halisi ya ESS Utumishi
Muonekano wa moja ya Tovuti Feki yenye sehemu ya kuweka username na password

Utapeli na Kughushi (Fraud):

Baadhi ya tovuti feki zinalenga kutoa taarifa za uongo kuhusu ajira, matangazo ya nafasi za kazi, au hata ‘kuuza’ huduma fulani zinazohusiana na ajira au mishahara. Wanaweza kuwataka watumiaji kulipa ada ndogo kwa ahadi ya kusaidiwa jambo fulani, jambo ambalo Serikali haifanyi kupitia ESS. Lengo la msingi ni kuiba pesa kutoka kwa watumishi.

Kujipatia Pesa Kwa Njia ya Matangazo

Sababu nyingine kubwa ya kuwepo kwa tovuti hizi feki ni kunasa trafiki (traffic) ya watumiaji na kuchanganya umma. Hili linafanyika kupitia mbinu ifuatayo:

Kutumia Majina Yanayofanana: Wahalifu wa mtandaoni huunda majina ya tovuti (domain names) ambayo yanafananana sana na jina halisi la ESS Utumishi. Wanaweza kuongeza herufi moja, kuondoa, au kutumia herufi zinazofanana kwa muonekano Kwa Mfano tovuti hizi zote zenye alama nyeupe ni feki.

Jinsi ya Kutambua Tovuti Halisi ya ESS Utumishi
Muonekano wa Baadhi ya Tovuti Feki Ukitafuta Kupitia Google

Tovuti hizi hazishii hapo pekee bali zipo nyingi sana na ni ngumu sana kwa mtu kuweza kujua kama wewe ni mtumiaji mgeni.

Jinsi ya Kutambua Tovuti Halisi

Ni muhimu sana kutumia tovuti/mfumo halisi wa ESS Utumishi. Kutumia mfumo halisi kwa mujibu wa serikali mfumo wa ESS utumishi unapatikana Kupitia kikoa hapo chini pekee na sio vinginevyo.

https://ess.utumishi.go.tz

Jinsi ya Kutambua Tovuti Halisi ya ESS Utumishi
Muonekano wa Tovuti halisi ya ESS Utumishi kupitia ess.utumishi.go.tz/sessions/signin

Tovuti halisi ya Serikali imejengwa kwa viwango vya juu vya usalama kulinda taarifa za watumishi. Taarifa zako za kibinafsi, za kazi, na za kifedha zitakuwa salama kutokana na wahalifu wa mtandaoni.

Mfumo halisi unatoa taarifa sahihi na za kisasa kuhusu mshahara wako, likizo, na mabadiliko yoyote katika sera au taratibu za utumishi.

Kupitia mfumo halisi, watumishi hutekeleza majukumu yao kama vile kujaza fomu za tathmini (Orodha ya Hati za Tathmini au Performance Appraisal Documents), kuomba likizo, au kupakua pay-slips zao. Matendo yote haya lazima yafanyike kwenye mfumo rasmi ili yaweze kutambulika na kutekelezwa na Serikali.

Jinsi ya Kuepuka Kutumia Tovuti Feki

Kujilinda ni muhimu, hivyo hakikisha unaangalia mambo yafuatayo kabla ya kuingiza taarifa zako:

  • Anwani Sahihi (URL): Anwani (URL) ya tovuti halisi ya ESS Utumishi inapaswa kuishia na .go.tz (government of Tanzania). Kwa mfano, anwani inayotumika kwa ESS ni ess.utumishi.go.tz Tovuti feki kwa kawaida hutumia anwani zenye makosa madogo ya herufi au hutumia viongezo visivyo rasmi kama vile .com, .org, .net, n.k.
  • Cheti cha Usalama (SSL Certificate): Hakikisha anwani ya tovuti inaanza na https:// na kuna alama ya kufuli (padlock icon) kando yake kwenye browser yako. Hii huonyesha kuwa tovuti imelindwa na mawasiliano yako ni siri.
  • Vyanzo Rasmi: Tumia viungo (links) vinavyotolewa kupitia Mamlaka ya Serikali ya Utumishi wa Umma au ofisi yako ya Rasilimali Watu (HR) badala ya kubofya viungo vinavyotumwa kupitia barua pepe au ujumbe mfupi usioutambua.

Kwa kuwa makini na kutumia tovuti halisi pekee, watumishi wa umma wanaweza kujikinga na ulaghai wa mtandaoni na kuhakikisha usalama wa taarifa zao za utumishi.

Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use