Popular Now
Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026 1

Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra 2

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini 3

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini

Apple Yatoa Toleo Jipya la iOS 11.2.6 Kwaajili ya Kuzuia Virusi 4

Apple Yatoa Toleo Jipya la iOS 11.2.6 Kwaajili ya Kuzuia Virusi

Hivi karibuni kuligundulika aina mpya ya virusi ambavyo vilikuwa na uwezo wa kuzuia programu mbalimbali za simu yako ya iphone kufanya kazi. Virusi hivyo vilivyokuwa vinatokana na neno la kihindi vinauwezo wa kuzima programu za ujumbe kama vile programu za iMassage, WhatsApp, Pamoja na FB Messenger.

Sasa hivi leo kampuni ya Apple imetoa toleo jipya la mfumo wa uendeshaji wa iOS 11.2.6 toleo ambalo litakuwa na uwezo wa kuondoa tatizo hilo pamoja na virusi hivyo. Hata hivyo Apple pia imetoa toleo jipya la mifumo ya vifaa vyake vingine kama watchOS, tvOS, pamoja na macOS.

Unaweza kuangalia update za kifaa chako sasa ili kuweza kulinda vifaa vyako vya Apple dhidi ya virusi hivyo vinavyotokana na neno la lugha ya kihindi (Telugu) . Kama unataka kuangalia update hizo, bofya sehemu ya Settings > alafu General > Software Update kisha download na install update hizo kwenye simu yako au vifaa vyenye kutumia mfumo wa watchOS, tvOS, pamoja na macOS.

Previous Post
Samsung Galaxy S9

Hizi Hapa Picha Nyingine za Simu Mpya ya Samsung Galaxy S9

Next Post
mabasi ya mwendokasi

Mabasi Mapya 70 ya Mwendokasi Yapokelewa Dar es Salaam